Aprili 7, 2020
Wakati mabilioni ya watu hawawezi kuwaona marafiki na familia zao ana kwa ana kwa sababu ya COVID-19, watu wanategemea kuwasiliana kwa WhatsApp zaidi kuliko wakati mwingine. Watu wanaongea na madaktari, waalimu, na wapendwa wao waliotengwa nao kwa kupitia WhatsApp wakati wa taharuki hii. Hiyo ndiyo sababu ujumbe na simu zako kwenye WhatsApp zimefumbwa kwa ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho kwa msingi ili kukupatia mahali salama pa mazungumzo yako binafsi.
Mwaka jana tuliwatambulisha watumiaji kwenye dhana ya ujumbe ambazo zimezambazwa mara nyingi. Ujumbe hizi zimepewa lebo ya mishale miwili
Kama huduma ya utumaji ujumbe wa kibinafsi, tumechukua hatua kadhaa kwa miaka zilizopita ili kukusaidia kuweka mazungumzo kuwa ya kisiri. Kwa mfano, mwanzoni tuliweka kikomo kwa usambazaji wa ujumbe ili kudhibiti kuenea haraka. Wakati huo, tuliona upungufu wa 25% kwa jumla wa usambazaji wa ujumbe ulimwenguni.
Je usambazaji wote ni mbaya? Kwa hakika hapana. Tunajua watumiaji wengi wanasambaza habari zinazosaidia, pamoja na video za kuchekesha, utani, na tafakari au maombi wanayoona kuwa ya maana. Katika wiki za hivi karibuni, watu pia wametumia WhatsApp kupanga wakati wa umma kuunga mkono wafanyakazi wa afya walio kwenye mstari wa mbele. Walakini, tumeona ongezeko kubwa katika kiwango cha usambazaji ambacho watumiaji wametuambia wanaweza kuhisi kuwa umezidi na unaweza kuchangia kuenea kwa habari potofu. Tunaamini ni muhimu kupunguza kasi ya kuenea kwa ujumbe hizi ili kuweka WhatsApp kuwa mahali pa mazungumzo ya kibinafsi.
Pamoja na mabadiliko haya, tunafanya kazi moja kwa moja na NGOs na serekali, pamoja na Shirika la Afya Duniani na wizara za afya za kitaifa zaidi ya 20, ili kusaidia kuunganisha watu na habari sahihi. Pamoja mamlaka hizi zinazoaminika zimetuma mamilioni ya ujumbe moja kwa moja kwa watu wanaoomba habari na ushauri. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu juhudi hizi, na jinsi ya kuwakilisha hadithi za uwongo, mzaha na uvumi kwenye mashirika ya kuchunguza ukweli, kwenye Kitovu chetu cha Habari za Virusi vya Corona.
Tunaamini kuwa sasa kuliko zamani watu wanahitaji kuunganishwa kibinafsi. Timu zetu zinafanya kazi sana ili kufanya WhatsApp iendelee kufanya kazi kwa ukamilifu wakati huu wa mgogoro ulimwenguni usiyo wa kawaida. Tutaendelea kusikiliza maoni yako na kuboresha njia ambazo watu wanaweza kushirikiana kwenye WatsApp.