Juni 15, 2020
Tunafurahi kutangaza kwamba kuanzia leo tunaleta malipo ya kidigitali kwa watumiaji wa WhatsApp Brazil. Watu wataweza kutuma pesa kwa usalama au kununa kutoka kwa biashara za ndani bila kuondoka kwenye soga zao.
Zaidi ya biashara ndogo na biashara maikro milioni 10 ni mapigomoyo ya jamii za Brazil. Inakuwa asili ya pili kutuma zap kwa biashara ili maswali yajibiwe. Sasa pamoja na kuona katalogi la duka, wateja wataweza pia kutuma malipo kwa ajili ya bidhaa. Kurahisisha malipo kunaweza kusaidia kuleta biashara zaidi kwenye uchumi wa kidigitali, na kufungua fursa mpya za ukuaji.
Zaidi ya hayo, tunafanya kutuma pesa kwa wapendwa kuwa rahisi kama kutuma ujumbe, jambo ambalo ni muhimu sana kwani watu wako mbali na wenzao. Kwa kuwa malipo kwenye WhatsApp yanawezeshwa na Facebook Pay, kwa siku za usoni tunataka kufanya uwezekano wa watu na biashara kutumia kadi hiyohiyo kwenye familia ya programu za Facebook.
Tumeunda malipo tukizingati usalama na PIN maalum ya tarakwimu sita au alama ya kidole itahitajika kuzuia miamala isiyoruhusiwa. Kwa kuanza, tutawezesha kadi za malipo au mikopo kutoka kwa Banco do Brasil, Nubank na Sicredi kwenye mitandao ya Visa na Mastercard -na tunafanya kazi na Cielo, kiongozi wa kichakataji cha malipo Brazil. Tumeunda modeli wazi kuwakaribisha washiriki zaidi siku za usoni.
Kutuma pesa au kununua kwenye WhatsApp ni bure kwa watu. Biashara zitalipa gharama za uchakataji ili kupokea malipo ya wateja, sawa na wanavyolipa tayari wanapokubali miamala ya kadi za mikopo.
Malipo kwenye WhatsApp yanaanza kusambazwa kote Brazil kuanzia leo na tunatarajia kuyaleta kwa wote tunavyoendelea mbele.