Machi 3, 2020
Tumefurahi sana kusasisha WhatsApp na kipengele ambacho kimeombwa sana na watumiaji wetu kila mahali - hali ya giza.
Hali ya giza ya WhatsApp inatoa mtazamo mpya kwa uzoefu unaoufahamu. Imeundwa kupunguza mnachuo wa jicho katika mazingira ya mwanga wa chini. Na tunatumaini itasaidia kuzuia nyakati zisizofaa ambako simu yako inatoa mwanga kwenye chumba.
Tulipokuwa tunaunda hali ya giza tulitumia muda kufanya utafiti na kuzingatia sehemu mbili maalum:
Usomaji: Wakati wa kuchagua rangi, tulitaka kupunguza uchofu wa jicho na kutumia rangi ambazo zinafanana na chaguo-msingi ya mfumo kwenye IPhone na Android.
Taarifa ya mfumo wa viwango: Tulitaka kuwasaidia watumiaji kuzingatia kwa urahisi umakini wao kwenye kila skrini. Tulifanya hivyo kwa kutumia rangi na vitu vingine vya muundo ili kuhakikisha kuwa habari muhimu zaidi inasisitizwa.
Watumiaji kwenye Android 10 na iOS 13 wanaweza kutumia hali ya giza kwa kuiwezesha katika mipangilio ya mfumo. Watumiaji kwenye Android 9 na chini wanaweza kuenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp > Soga > Mandhari > chagua ‘Giza’.
Tunatumahi kuwa kila mtu anafurahia hali ya giza, ambayo inajitokeza katika siku zijazo kwenye toleo la hivi karibuni la WhatsApp.