WhatsApp Blog
Chagua lugha yako
  • azərbaycan
  • Afrikaans
  • Bahasa Indonesia
  • Melayu
  • català
  • čeština
  • dansk
  • Deutsch
  • eesti
  • English
  • español
  • français
  • Gaeilge
  • hrvatski
  • italiano
  • Kiswahili
  • latviešu
  • lietuvių
  • magyar
  • Nederlands
  • norsk bokmål
  • o‘zbek
  • Filipino
  • polski
  • Português (Brasil)
  • Português (Portugal)
  • română
  • shqip
  • slovenčina
  • slovenščina
  • suomi
  • svenska
  • Tiếng Việt
  • Türkçe
  • Ελληνικά
  • български
  • қазақ тілі
  • македонски
  • русский
  • српски
  • українська
  • עברית
  • العربية
  • فارسی
  • اردو
  • বাংলা
  • हिन्दी
  • ગુજરાતી
  • ಕನ್ನಡ
  • मराठी
  • ਪੰਜਾਬੀ
  • தமிழ்
  • తెలుగు
  • മലയാളം
  • ไทย
  • 简体中文
  • 繁體中文
  • 日本語
  • 한국어
  • WhatsApp Web
  • Vipengele
  • Pakua
  • Usalama
  • Kituo cha Msaada
  • Pakua
  • Vipengele
  • Usalama
  • Kituo cha Msaada
  • Kuwa karibu

WhatsApp Blog

Kuanzisha vibandiko vilivyohuishwa, misimbo ya QR na zaidi

Tayari WhatsApp inatumiwa na kupendwa na watu zaidi ya bilioni 2 kote duniani. Wakati mwelekeo wetu unabakia kuwa njia rahisi, ya kuaminika na ya faragha kwa watu kupiga soga na marafiki na familia - sisi pia tunaendelea kusukuma mbele muundo wetu wa bidhaa ili kuhakikisha kuwa WhatsApp inabaki kuwa njia bora kwa mtu yeyote, mahali popote kujiunga.

Leo, tunafurahia kuthibitisha baadhi ya vipengele vipya ambavyo vinatolewa kwa muda wa wiki chache zijazo:

  • Vibandiko Vilivyohuishwa: Vibandiko ni njia moja inayokua haraka ambayo watu wanawasiliana kwenye WhatsApp, na bilioni zikiwa zinatumwa kila siku. Tunatoa vifurushi vipya vya vibandiko vilivyohuishwa vitafurahisha zaidi na kujieleza zaidi.
  • Misimbo ya QR: Tunafanya kuongeza mwasiliani mpya kuwa rahisi zaidi kuliko awali. Hivi karibuni utakapokutana na watu wapya, utaweza kukagua msimbo wao wa QR na kuwaongeza kwenye waasiliani wako. Hakuna tena kuandika tarakimu zao moja baada ya nyingine.
  • Hali ya Giza ya WhatsApp Web na Desktop: Mandhari ya Hali ya Giza iliyo maarufu sana sasa inaenea kwa kompyuta yako.
  • Uboreshaji wa simu za video za kikundi: Kwa sasa hadi watu 8 kwenye simu ya video, tumefanya kuwe rahisi kuzingatia mtu yeyote unayetaka kwa kukuruhusu ubonyeze na ushikilie kutanua video ya mshiriki ili iwe skrini kamilifu. Pia tumeongeza aikoni ya video kwenye soga za kikundi cha watu 8 au pungufu, ili uweze kuanzisha simu ya video ya kikundi kwa mguso 1.
  • Hali inakuja kwa KaiOS: Watumiaji wa KaiOS wanaweza sasa kufurahia kipengele maarufu kinachoruhusu kushirikisha sasisho ambazo zinatoweka baada ya masaa 24.

Vipengele hivi vinatolewa kwa watumiaji kwa muda wa wiki chache zijazo, kwenye toleo la hivi karibuni la WhatsApp.

Julai 1, 2020
Tweet
Kuleta Malipo ya WhatsApp kwa Watu na Biashara Ndogo Brazil

Tunafurahi kutangaza kwamba kuanzia leo tunaleta malipo ya kidigitali kwa watumiaji wa WhatsApp Brazil. Watu wataweza kutuma pesa kwa usalama au kununa kutoka kwa biashara za ndani bila kuondoka kwenye soga zao.

Zaidi ya biashara ndogo na biashara maikro milioni 10 ni mapigomoyo ya jamii za Brazil. Inakuwa asili ya pili kutuma zap kwa biashara ili maswali yajibiwe. Sasa pamoja na kuona katalogi la duka, wateja wataweza pia kutuma malipo kwa ajili ya bidhaa. Kurahisisha malipo kunaweza kusaidia kuleta biashara zaidi kwenye uchumi wa kidigitali, na kufungua fursa mpya za ukuaji.

Zaidi ya hayo, tunafanya kutuma pesa kwa wapendwa kuwa rahisi kama kutuma ujumbe, jambo ambalo ni muhimu sana kwani watu wako mbali na wenzao. Kwa kuwa malipo kwenye WhatsApp yanawezeshwa na Facebook Pay, kwa siku za usoni tunataka kufanya uwezekano wa watu na biashara kutumia kadi hiyohiyo kwenye familia ya programu za Facebook.

Tumeunda malipo tukizingati usalama na PIN maalum ya tarakwimu sita au alama ya kidole itahitajika kuzuia miamala isiyoruhusiwa. Kwa kuanza, tutawezesha kadi za malipo au mikopo kutoka kwa Banco do Brasil, Nubank na Sicredi kwenye mitandao ya Visa na Mastercard -na tunafanya kazi na Cielo, kiongozi wa kichakataji cha malipo Brazil. Tumeunda modeli wazi kuwakaribisha washiriki zaidi siku za usoni.

Kutuma pesa au kununua kwenye WhatsApp ni bure kwa watu. Biashara zitalipa gharama za uchakataji ili kupokea malipo ya wateja, sawa na wanavyolipa tayari wanapokubali miamala ya kadi za mikopo.

Malipo kwenye WhatsApp yanaanza kusambazwa kote Brazil kuanzia leo na tunatarajia kuyaleta kwa wote tunavyoendelea mbele.

Juni 15, 2020
Tweet
Video na Simu za Kikundi Sasa Zinawezesha Washiriki 8

Janga la COVID-19 limemaanisha kwamba wengi wetu sasa tumetenganishwa na marafiki na familia. Matokeo yake, tunaona kwamba watu kote ulimwenguni wanageukia upigaji simu na video kwenye WhatsApp zaidi kuliko hapo awali. Simu za kikundi zimekuwa muhimu sana na watumiaji wetu wameuliza kuungana na watu wengi kwa mara moja. Kuanzia leo, tunaongeza mara mbili zaidi ya idadi ya washiriki unaoweza kuwa nao kwenye video au simu ya WhatsApp kutoka watu 4 hadi 8 kwa wakati mmoja.

Kwa mwezi uliopita, kwa wastani watu wametumia zaidi ya dakika bilioni 15 wakiongea kila siku kwenye simu za WhatsApp, ikiwa ni zaidi ya siku ya kawaida kabla ya janga. Na kama ilivyo kwenye ujumbe wa maandishi, simu hizo zote zimelindwa kwa ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho. Tumeunda upigaji simu wa kikundi kwa njia ambayo inafanya ipatikane kwa watumiaji wengi iwezekanavyo, ikiwa ni pamoja na watu wenye vifaa vya viwango vya chini na muunganisho wa kasi ya chini wa mtandao.

Tunajua watu wanaweza kuhitaji njia mbalimbali za kujiunga wakati wakiwa nyumbani, hiyo ndiyo sababu WhatsApp pia inapatikana kwenye Portal — ambayo watumiaji wengi wametuambia imekuwa njia nzuri ya kushiriki sebule zao na familia wakati huu wa karantini.

Kupata WhatsApp mpya, yenye kipimo cha juu cha washiriki kwenye simu za WhatsApp, washiriki wote kwenye simu wanahitajika kusasisha toleo la hivi karibuni la WhatsApp linalopatikana kwenye iPhone au Android leo. Waulize marafiki zako na familia kusasisha WhatsApp na kuijaribu.

Aprili 28, 2020
Tweet
Kukaa umeunganishwa kupitia Vibandiko

Mabilioni ya vibandiko vinatumwa kila siku kwenye WhatsApp ili kuwasaidia watu kushiriki mawazo ya faragha na hisia bila ya kuandika hata neno moja. Tangu tulipozindua vibandiko miezi 18 iliyopita, vimekuwa mojawapo ya njia zinazokua kwa kasi za watu kuwasiliana kwenye WhatsApp.

Tunafurahia kufanya kazi na Shirika la Afya Duniani kuanzisha kifurushi cha kibandiko cha "Pamoja Nyumbani" ambacho kitawasaidia watu kuunganishwa wakati wote wa janga kubwa la COVID-19 na hata baadaye. Vibandiko kama hivi vinaweza kuwa vya kufurahisha, kuelemisha na vya kijumla, kuvunja vizuizi vya lugha, umri, na vingine.

Tunatumaini watu watafurahia kutumia vibandiko hivi kuwajulia hali wapendwa wao, haswa wale wanaojisikia wametengwa, wapweke na kuogopa. Kifurushi hiki kinatoa namna ya ubunifu ya kuwakumbusha watu kuosha mikono yao, kudumisha umbali, mazoezi na muhimu pia kusherehekea mashujaa wa matibabu na vilevile mashujaa wa kibinafsi katika maisha yetu.

Kifurushi cha kibandiko cha "Pamoja Nyumbani" sasa kinapatikana kwenye WhatsApp, ikiwa ni pamoja na maandishi kwenye lugha 9 - Kiarabu, Kifaransa, Kijerumani, Kiindonesia, Kiitaliano, Kireno, Kirusi, Kihispania na Kituruki.

Aprili 21, 2020
Tweet
Kuweka WhatsApp iwe ya Kibinafsi na ya Faragha

Wakati mabilioni ya watu hawawezi kuwaona marafiki na familia zao ana kwa ana kwa sababu ya COVID-19, watu wanategemea kuwasiliana kwa WhatsApp zaidi kuliko wakati mwingine. Watu wanaongea na madaktari, waalimu, na wapendwa wao waliotengwa nao kwa kupitia WhatsApp wakati wa taharuki hii. Hiyo ndiyo sababu ujumbe na simu zako kwenye WhatsApp zimefumbwa kwa ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho kwa msingi ili kukupatia mahali salama pa mazungumzo yako binafsi.

Mwaka jana tuliwatambulisha watumiaji kwenye dhana ya ujumbe ambazo zimezambazwa mara nyingi. Ujumbe hizi zimepewa lebo ya mishale miwili kuonyesha hazikuanzishwa na mwasiliani wako wa karibu. Kwa kweli, ujumbe hizi sio za kibinafsi zikilinganishwa na ujumbe wa kawaida zilizotumwa kwenye WhatsApp. Sasa tunaanzisha kikomo ili ujumbe zisambazwe tu kwenye soga moja kwa wakati mmoja.

Kama huduma ya utumaji ujumbe wa kibinafsi, tumechukua hatua kadhaa kwa miaka zilizopita ili kukusaidia kuweka mazungumzo kuwa ya kisiri. Kwa mfano, mwanzoni tuliweka kikomo kwa usambazaji wa ujumbe ili kudhibiti kuenea haraka. Wakati huo, tuliona upungufu wa 25% kwa jumla wa usambazaji wa ujumbe ulimwenguni.

Je usambazaji wote ni mbaya? Kwa hakika hapana. Tunajua watumiaji wengi wanasambaza habari zinazosaidia, pamoja na video za kuchekesha, utani, na tafakari au maombi wanayoona kuwa ya maana. Katika wiki za hivi karibuni, watu pia wametumia WhatsApp kupanga wakati wa umma kuunga mkono wafanyakazi wa afya walio kwenye mstari wa mbele. Walakini, tumeona ongezeko kubwa katika kiwango cha usambazaji ambacho watumiaji wametuambia wanaweza kuhisi kuwa umezidi na unaweza kuchangia kuenea kwa habari potofu. Tunaamini ni muhimu kupunguza kasi ya kuenea kwa ujumbe hizi ili kuweka WhatsApp kuwa mahali pa mazungumzo ya kibinafsi.

Pamoja na mabadiliko haya, tunafanya kazi moja kwa moja na NGOs na serekali, pamoja na Shirika la Afya Duniani na wizara za afya za kitaifa zaidi ya 20, ili kusaidia kuunganisha watu na habari sahihi. Pamoja mamlaka hizi zinazoaminika zimetuma mamilioni ya ujumbe moja kwa moja kwa watu wanaoomba habari na ushauri. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu juhudi hizi, na jinsi ya kuwakilisha hadithi za uwongo, mzaha na uvumi kwenye mashirika ya kuchunguza ukweli, kwenye Kitovu chetu cha Habari za Virusi vya Corona.

Tunaamini kuwa sasa kuliko zamani watu wanahitaji kuunganishwa kibinafsi. Timu zetu zinafanya kazi sana ili kufanya WhatsApp iendelee kufanya kazi kwa ukamilifu wakati huu wa mgogoro ulimwenguni usiyo wa kawaida. Tutaendelea kusikiliza maoni yako na kuboresha njia ambazo watu wanaweza kushirikiana kwenye WatsApp.

Aprili 7, 2020
Tweet
Hali ya giza sasa inapatikana kwa iPhone na Android

Tumefurahi sana kusasisha WhatsApp na kipengele ambacho kimeombwa sana na watumiaji wetu kila mahali - hali ya giza.

Hali ya giza ya WhatsApp inatoa mtazamo mpya kwa uzoefu unaoufahamu. Imeundwa kupunguza mnachuo wa jicho katika mazingira ya mwanga wa chini. Na tunatumaini itasaidia kuzuia nyakati zisizofaa ambako simu yako inatoa mwanga kwenye chumba.

Tulipokuwa tunaunda hali ya giza tulitumia muda kufanya utafiti na kuzingatia sehemu mbili maalum:

Usomaji: Wakati wa kuchagua rangi, tulitaka kupunguza uchofu wa jicho na kutumia rangi ambazo zinafanana na chaguo-msingi ya mfumo kwenye IPhone na Android.

Taarifa ya mfumo wa viwango: Tulitaka kuwasaidia watumiaji kuzingatia kwa urahisi umakini wao kwenye kila skrini. Tulifanya hivyo kwa kutumia rangi na vitu vingine vya muundo ili kuhakikisha kuwa habari muhimu zaidi inasisitizwa.

Watumiaji kwenye Android 10 na iOS 13 wanaweza kutumia hali ya giza kwa kuiwezesha katika mipangilio ya mfumo. Watumiaji kwenye Android 9 na chini wanaweza kuenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp > Soga > Mandhari > chagua ‘Giza’.

Tunatumahi kuwa kila mtu anafurahia hali ya giza, ambayo inajitokeza katika siku zijazo kwenye toleo la hivi karibuni la WhatsApp.

Machi 3, 2020
Tweet
Watumiaji Bilioni Mbili -- Kuunganisha Ulimwengu Kifaragha

Tumefurahi kuwaeleza kwamba, kama ya leo, WhatsApp inasaidia zaidi ya watumiaji bilioni mbili duniani kote.

Akina mama na akina baba wanaweza kuwapata wapendwa wao popote walipo. Akina kaka na dada wanaweza kushirikisha muda muhimu. Wafanyakazi wanaweza kushirikiana, na biashara inaweza kukua kwa kuunganisha kirahisi na wateja wao.

Mazungumzo ya kibinafsi ambayo wakati mmoja yaliwezekana tu kwa ana-kwa-ana sasa zinaweza kufanyika katika umbali mkubwa kupitia soga za papo hapo na simu ya video. Kuna wakati mwingi muhimu na maalum ambayo yanafanyika kwenye WhatsApp na tunajinyenyekea na kupokea heshima ya kufikia hatua hii kuu.

Tunajua kwamba tunavyoungana zaidi, ndvyo tunavyohitaji kulinda zaidi. Tunapoendesha zaidi maisha yetu mtandaoni, kulinda mazungumzo yetu ni muhimu zaidi kuliko hapo awali.

Ndiyo sababu kila ujumbe wa kibinafsi uliotumwa kwa kutumia WhatsApp umelindwa kimsingi na ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho. Ufumbaji imara ni kama kufuli ya kidijitali ambacho hakiwezi kuvunjwa na kinaweka maelezo unayotuma kwa kupitia WhatsApp salama, kukusaidia kukulinda kutoka kwa wadadisi na wahalifu. Ujumbe huhifadhiwa tu kwenye simu yako, na hakuna mtu kati anayeweza kusoma ujumbe wako au kusikiliza simu zako, hata sisi. Mazungumzo yako ya kibinafsi yanakaa kati yenu.

Ufumbaji imara ni jambo la lazima katika maisha ya kisasa. Hatutakiuka juu ya usalama kwa sababu kufanya hivyo kutafanya watu kupungukiwa kidogo na usalama. Ili kuwa na usalama zaidi, tunafanya kazi na wataalam wa hali ya juu wa usalama, kutumia teknolojia inayoongoza kusimamisha matumizi mabaya na vile vile kutoa udhibiti na njia za kuripoti maswala — bila kupunguza faragha.

WhatsApp ilianza na lengo la kuunda huduma ambayo ni rahisi, ya kuaminika, na ya faragha kwa watu kutumia. Leo tunabaki tumejitolea kama vile tulipoanza, kusaidia kuunganisha ulimwengu kifaragha na kulinda mawasiliano ya kibinafsi ya watumiaji bilioni mbili ulimwenguni.

Februari 12, 2020
Tweet
Kutambulisha Orodha za Biashara Ndogo

Watu wanapenda kupiga soga kwenye WhatsApp na biashara wanazopendelea, lakini kubadilishana jumbe na picha nyingi ili kupata maelezo ya bidhaa kunachosha. Leo tuna rahisisha kujifunza kuhusu bidhaa na huduma biashara zinazotoa kwa kutambulisha orodha kwenye programu ya WhatsApp Business.

Orodha ni rafu ya duka rununu kwa ajili ya biashara kuonyesha na kushirikisha bidhaa zao ili watu wanaweza kuvinjari kwa urahisi na kugundua kitu ambacho wangependa kununua. Zamani biashara zililazimika kutuma picha za bidhaa moja kwa wakati mmoja na kurudia kutoa maelezo - sasa wateja wanaweza kuona orodha yao kamili kwenye WhatsApp. Hii inawafanya wamiliki wa biashara waonekane kitaalamu zaidi na inawafanya wateja kujiingiza kwenye soga bila kutembelea tovuti.

Kama Agradaya, biashara endelevu ya mimea na viungo iliyo Indonesia. Tulimpa mwanzilishi Andhika Mahardika ufikiaji wa kipengele cha orodha mapema na alituambia kwamba kinafanya wateja wajifunze kirahisi kuhusu bidhaa zao, kujua bei na kuona picha za wanazotoa - hii ni muhimu kwa kuwahudumia wateja wao kwa ubora.

Kwa kila kitu kwenye orodha, biashara inaweza kuongeza habari pamoja na bei, maelezo na nambari ya bidhaa. WhatsApp inahudumia orodha hizi ili kuokoa nafasi muhimu ya hifadhi kwenye simu za biashara na wateja wote.

Kuunda orodha kwenye programu ya WhatsApp Business inachukua tu hatua chache. Tazama video ili kuanza:


Kipengele hiki cha orodha kinapatikana leo kwa biashara zinazotumia programu ya WhatsApp Business kwenye Android na iPhone nchini Brazil, Ujerumani, India, Indonesia, Mexico, Uingereza na Marekani. Itatandazwa duniani kote hivi karibuni. Hatuwezi kungojea kusikia jinsi orodha zinasaidia biashara ndogo kuungana na wateja wao na kukua.

Novemba 7, 2019

Tweet
Kutambulisha Kufuli cha Alama ya Kidole kwa Android

Mapema mwaka huu, tulizindua Touch ID na Face ID kwa iPhone ili kutoa safu ya ziada ya usalama kwa watumiaji wa WhatsApp. Leo, tunatambulisha uthibitishaji kama huo,unaokuruhusu kufungua programu na alama ya kidole chako, kwa simu za Android zilizowezeshwa. Kuiwezesha, gusa Mipangilio > Akaunti > Faragha > Kufuli cha alama ya kidole. Kuwasha Fungua na alama ya kidole, na thibitisha alama ya kidole chako.

Oktoba 31, 2019
Tweet
Mipangilio Mipya ya Faragha ya Vikundi

Vikundi vya WhatsApp vinaendelea kukuunganisha na familia, marafiki, wafanyakazi wenzako, wanafunzi wenzako, na zaidi. Vile watu wanavyotumia vikundi kwa mazungumzo muhimu, watumiaji wameomba udhibiti zaidi juu ya uzoefu wao. Leo, tunatambulisha mpangilio wa faragha mpya na mfumo wa kualika ili kukusaidia kuamua ni nani anayeweza kukuongeza kwenye vikundi.

Kuiwezesha, nenda kwenye Mipangilio ya programu yako, kisha gusa Akaunti > Faragha > Vikundi na chagua mojawapo ya hiari tatu: “Kila Mtu,” “Waasiliani Wangu,” au “Waasiliani Wangu Isipokua.” “Waasiliani Wangu” inamaanisha kuwa watumiaji tu waliopo kwenye kitabu chako cha anwani ndiyo wanaoweza kukuongeza kwenye vikundi na “Waasiliani Wangu Isipokuwa” hutoa udhibiti wa ziada kwa nani miongoni mwa waasiliani wako wanaweza kukuongeza kwenye kikundi.

Kwenye kesi hizo, mtawala ambaye hawezi kukuongeza kwenye kikundi atatakiwa kutuma mwaliko wa faragha kwa kupitia soga ya kibinafsi, kukupa hiari ya kujiunga na kikundi hicho. Utakuwa na siku tatu za kukubali mwaliko kabla ya muda wake kuisha.

Kwa vipengele hivi vipya, watumiaji watakuwa na udhibiti zaidi wa jumbe za kikundi wanazopokea. Mipangilio hii mpya ya faragha itaanza kuwezeshwa kwa watumiaji wengine kuanzia leo na itakuwa inapatikana duniani kote katika siku zijazo kwa wale wanaotumia toleo la karibuni la WhatsApp.

SASISHO: Kulingana na maoni kutoka kwa watumiaji wakati wa usambazaji wetu wa awali, badala ya chaguo la "Hakuna mtu" sasa tunatoa hiari ya “Waasiliani Wangu Isipokuwa”. Hii inakuwezesha kuchagua kutenganisha waasiliani maalum au "chagua wote". Sasisho hili linasambaziwa kwa watumiaji duniani kote kwenye toleo la hivi karibuni la WhatsApp.

Mwisho Ilisasishwa: Novemba 5, 2019

Aprili 3, 2019
Tweet
Ukurasa Unaofuata

WhatsApp

  • Vipengele
  • Usalama
  • Pakua
  • WhatsApp Web
  • Biashara
  • Faragha

Shirika

  • Kuhusu
  • Kazi
  • Kituo cha Bidhaa
  • Kuwa karibu
  • Blog
  • Hadithi za WhatsApp

Pakua

  • Mac/PC
  • Android
  • iPhone

Msaada

  • Kituo cha Msaada
  • Twitter
  • Facebook
  • Virusi vya Korona
2021 © WhatsApp LLC
Faragha na Masharti