WhatsApp inafahari kuzindua kifurushi kipya cha vibandiko kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) kinachoitwa “Vaccines for All.” Tunataraji kwamba vibandiko hivi vitawapa watu njia bunifu na ya kupendeza ya kuwasiliana na kueleza furaha, utulivu na matumaini wanayohisi kwa faragha kwa kuzingatia yanayowezekana kutokana na chanjo ya COVID-19 pamoja na kuonyesha shukrani zao kwa wahudumu wa afya ambao wameendelea na ushujaa wa kuokoa maisha katika kipindi hiki kirefu kigumu.
Tangu kuanza kwa janga hili, tumeshirikiana na zaidi ya mashirika 150 ya kitaifa, majimbo na serikali za mitaa, pamoja na mashirika kama vile WHO na UNICEF kutoa huduma za COVID-19 kwa njia ya simu ili kuwaunganisha zaidi ya watumiaji bilioni 2 na taarifa na nyenzo sahihi. Zaidi ya ujumbe bilioni 3 umetumwa kupitia nambari hizi za huduma kote duniani katika mwaka uliopita.
Kwa vile janga linaingia katika awamu mpya katika mataifa mengi, serikali zinatumia nambari hizi za huduma kwa simu ili kuwaunganisha raia na taarifa sahihi za chanjo na usajili kwa njia ya faragha katika mataifa kama vile Indonesia, Afrika Kusini, Argentina, Brazil na India. Nchini Indonesia, wafanyakazi 500,000 wa afya walijisajili kwa miadi yao ya chanjo kupitia huduma hii katika siku 5 za kwanza.
Tunataka kusaidia serikali na mashirika ya kimataifa kuwaunganisha watu wengi kote duniani na taarifa na huduma za chanjo kadri inavyowezekana, hasa katika maeneo yaliyo magumu kufikia au miongoni mwa makundi ya waliotengwa. Pia tumeondoa matozo yanayotokana na utumaji wa ujumbe kupitia API ya WhatsApp Business.
Tunapoendelea polepole kurejelea utangamano wa ana kwa ana katika baadhi ya nchi, tunataraji kwamba watu wataendelea kushiriki mawazo na hisia zao za faragha - pamoja na matumaini - na ndugu na marafiki zao wa karibu kwenye WhatsApp.
Kifurushi cha vibandiko vya “Vaccines for All” sasa kinapatikana kwenye WhatsApp.
Ni fahari yetu kukutangazia kwamba njia salama na ya faragha ya kupiga simu za sauti na video kati ya mtu na mwingine sasa inapatikana kwenye programu ya WhatsApp kwenye kompyuta.
Katika mwaka uliopita, tumeshuhudia ongezeko la watu wanaopigiana simu kwenye WhatsApp, aghalabu kwa mazungumzo ya muda mrefu. Katika Mkesha wa Mwaka Mpya mwaka jana, tulivunja rekodi kwa kuwa na simu bilioni 1.4 za sauti na video zilizopigwa katika siku moja pekee. Huku kukiwa na idadi kubwa ya watu ambao bado wapo mbali na wapendwa wao na kuendelea kuzoelea njia mpya za kufanya kazi, tunataka mazungumzo kwenye WhatsApp yahisi kana kwamba ni ya ana kwa ana kadiri iwezekanavyo, bila kujali mahali ulipo ulimwenguni au ni teknolojia gani unatumia.
Kupokea simu katika skrini kubwa kunarahisisha kufanya kazi na wafanyakazi wenzako, kuwaona wanafamilia kwa ubora zaidi kwenye kiwambo kikubwa, au kukuruhusu kutumia mikono yako kufanya vitu vingine wakati unazungumza. Ili kufanya upigaji simu kwenye kompyuta uwe na manufaa zaidi, tumehakikisha kwamba inafanya kazi vizuri katika mkao wima au mlazo, inaonekana kwenye kidirisha huru kinachoweza kubadili ukubwa wake kwenye skrini ya kompyuta yako, na ambacho kitakuwa katika sehemu ya juu ya skrini kila wakati ili usipoteze soga zako za video kwenye kichupo cha kivinjari au katika madirisha uliyofungua.
Simu za sauti na video kwenye WhatsApp hufumbwa mwisho hadi mwisho, kwa hivyo WhatsApp haiwezi kuzisikia au kuziona, iwe unapiga kutoka kwenye simu au kompyuta yako. Tunaanza kwa simu za mtu na mwenzake katika programu ya WhatsApp kwenye kompyuta ili kuhakikisha kwamba tunakupa huduma ya hali ya juu. Tutapanua kipengele hiki ili kujumuisha simu za sauti na za video kwa ajili ya vikundi katika siku zijazo.
Ni matarajio yetu kwamba watu watafurahia kuwapigia ndugu na marafiki zao simu kwa njia salama na ya faragha kwenye kompyuta. Unaweza kusoma zaidi, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kupakua programu ya kompyuta kwa ajili ya Windows na Mac hapa.
Leo tunashiriki mipango iliyosasishwa kuhusu jinsi tutakavyowaomba watumiaji wa WhatsApp kuhakiki masharti yetu ya huduma na sera ya faragha. Hapo awali tulikabiliana na kiasi kikubwa cha taarifa zisizofaa kuhusu sasisho hili na tunazidi kujitahidi ili kuondoa mkanganyiko wowote.
Kumbuka, tunatengeneza njia mpya za kuwasiliana au kununua katika biashara zilizo kwenye WhatsApp, ni hiari kabisa kutumia njia hizo. Ujumbe wa binafsi utaendelea kufumbwa mwisho hadi mwisho kila wakati, kumaanisha kwamba WhatsApp haiwezi kusikia au kuusoma.
Tumetafakari kuhusu kile tungefanya kwa njia tofauti. Tungependa kila mtu ajue historia yetu ya kutetea ufumbaji wa mwisho hadi mwisho na aamini kwamba tumejitolea kulinda faragha na usalama wa watu. Sasa tunatumia sehemu ya Hali kushiriki maadili na masasisho yetu moja kwa moja kwenye WhatsApp. Tutafanya zaidi ili kuhakikisha kwamba tunaeleweka vizuri siku za usoni.
Katika wiki chache zijazo, tutaonyesha bango kwenye WhatsApp likiwa na maelezo zaidi ambayo watu wanaweza kuyasoma kwa wakati wao wenyewe. Pia tumejumuisha maelezo zaidi ili kujaribu kushughulikia baadhi ya madukuduku ambayo tunayasikia. Hatimaye, tutaanza kuwakumbusha watu wakague na kukubali masasisho haya ili waweze kuendelea kutumia WhatsApp.
Pia tunadhani ni muhimu kwa watu kujua jinsi tunavyoweza kutoa huduma za WhatsApp bila malipo. Kila siku, mamilioni ya watu huanzisha soga ya WhatsApp ili kuwasiliana na biashara kwa sababu ni rahisi zaidi ya kupiga simu au kuandikiana barua pepe. Tunatoza biashara ili ziweze kutoa huduma kwa wateja kwenye WhatsApp - hatutozi watu. Baadhi ya vipengele vya ununuzi huhusisha Facebook ili biashara ziweze kudhibiti orodha zao za bidhaa kwenye programu hizi. Tunaonyesha maelezo zaidi moja kwa moja kwenye WhatsApp ili watu waweze kuchagua ikiwa wanataka kuingiliana na biashara, au la.
Katika kipindi hiki, tunaelewa kwamba baadhi ya watu wanaweza kuangalia programu nyingine zilivyo. Tumeshuhudia baadhi ya washindani wetu wakijaribu kudai kwamba hawawezi kuona mawasiliano ya watu - ikiwa programu haina ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwa chaguomsingi, basi inaweza kusoma ujumbe wako. Baadhi ya programu zinadai kwamba ni bora kwa sababu zina taarifa chache ikilinganishwa na WhatsApp. Tunaamini kwamba watu wanataka programu ziwe salama na za uhakika, hata kama hilo linamaana kwamba WhatsApp itahitaji kiasi fulani cha data. Tunajitahidi kuwa waangalifu katika uamuzi tunaofanya na tutaendelea kubuni njia mpya za kutimiza majukumu haya kwa kutumia taarifa chache, si nyingi.
Tunamshukuru kwa dhati kila mtu ambaye ametusaidia kushughulikia changamoto hizi na bado tupo tayari kujibu maswali yoyote. Hatujaacha kubuni kwa ajili ya 2021 na tunatarajia tutakuwa na mengi ya kushiriki katika wiki na miezi ijayo.
Tumesikia kutoka kwa watu wengi jinsi ambavyo kuna mkanganyiko kuhusu sasisho letu la hivi karibuni. Kuna taarifa potofu zinazosababisha wasiwasi na tunataka kusaidia kila mmoja aelewe kanuni zetu na ukweli.
WhatsApp ilijengwa kwa kuzingatia wazo rahisi: unachoshiriki na familia na marafiki zako hukaa kati yenu. Hii ina maana kwamba huwa tunalinda mazungumzo yenu ya binafsi kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kila wakati, hivi kwamba WhatsApp wala Facebook haziwezi kuona ujumbe wenu wa faragha. Ndiyo maana hatuweki kumbukumbu ya watu wanaotumiwa ujumbe au kupigiwa simu. Pia hatuwezi kuona mahali unapopashiriki na hatuwezi kushiriki waasiliani wako na Facebook.
Kwenye masasisho haya, hayo yote hayabadiliki. Badala yake, sasisho linajumuisha hiari mpya ambazo watu watakuwa nazo ili kutumia biashara ujumbe kwenye WhatsApp na linatoa uwazi zaidi kuhusu jinsi tunavyokusanya na kutumia data. Japo si kila mtu ananunua kutoka kwenye biashara inayotumia WhatsApp kwa sasa, tunadhani kwamba watu wengi watachagua kufanya hivyo siku za baadaye na ni muhimu watu wajue uwepo wa huduma hizi. Sasisho hili haliongezi uwezo wetu wa kushiriki data na Facebook.
Sasa tunasogeza mbele tarehe ambayo watu wataulizwa kuhakiki na kukubali masharti husika. Hakuna mtu atasitishiwa au kufutiwa akaunti yake tarehe 8 Februari. Tutaendeleza zaidi juhudi za kusahihisha taarifa potofu kuhusu jinsi faragha na usalama vinavyofanya kazi kwenye WhatsApp. Kisha tutawaendea watu taratibu ili waweze kuhakiki sera kwa mwendo wao wenyewe kabla ya kuanza kutumika kwa chaguo mpya za biashara tarehe 15 Mei.
WhatsApp ilisaidia kuleta ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwa watu kote duniani na tumejitolea kutetea teknolojia hii ya usalama sasa na baadaye. Shukrani kwa kila mmoja ambaye amewasiliana nasi na wengi ambao wamesaidia kusambaza ukweli na kukomesha uvumi. Tutaendelea kufanya kila tuwezalo ili kuboresha WhatsApp iwe njia bora ya kuwasiliana kwa faragha.
WhatsApp inazidi kuwa jukwaa ambapo watu hujadili kuhusu bidhaa na kuratibu mauzo. Katalogi zimewasaidia watu kuona kwa haraka bidhaa zinazopatikana na kuzisaidia biashara kupanga soga zao ili kuambatana na bidhaa mahususi. Huku idadi ya ununuzi unaofanyika kupitia soga ikiendelea kuongezeka, tunataka kufanya mchakato wa ununuzi na uuzaji kuwa rahisi zaidi.
Kuanzia leo, ni fahari yetu kukuletea vikapu kwenye WhatsApp. Vikapu ni kipengele kizuri unapotuma ujumbe kwa biashara ambayo inauza bidhaa nyingi kwa mkupuo, kwa mfano, mkahawa au duka la nguo. Kwa kutumia vikapu, watu wanaweza kuvinjari katalogi, kuchagua bidhaa kadhaa na kutuma oda ikiwa ujumbe mmoja kwenda kwa biashara. Hatua hii itazirahisishia biashara kufuatilia maswali ya oda, kudhibiti maombi ya wateja na kufanya mauzo.
Kwa mfano, Agradaya, biashara endelevu ya mimea na manukato huko Yogyakarta, Indonesia ilipata ufikiaji wa mapema wa huduma hiyo na kutuambia jinsi vikapu ni njia rahisi ya kuelewa kile mteja anachoagiza bila mawasiliano ya mara kadhaa.
Ni rahisi kutumia vikapu. Tafuta tu bidhaa unazotaka kisha uguse “weka kwenye kikapu”. Ukishaweka vitu unavyohitaji kwenye kikapu, kitume kama ujumbe kwenda kwa biashara. Maelezo zaidi juu ya kutumia vikapu yanaweza kupatikana hapa.
Kipengele cha vikapu kitaanza kutumika kote duniani kuanzia leo -- wakati mwafaka kwa ajili ya msimu wa sikukuu. Furahia ununuzi kwenye WhatsApp!
Kuanzia leo, watu kote nchini India wataweza kutuma pesa kupitia WhatsApp. Njia hii salama ya malipo inafanya shughuli ya kuhamisha pesa iwe rahisi tu kama kutuma ujumbe. Watu wanaweza kutuma pesa kwa familia zao kwa usalama au kuchangia gharama za bidhaa bila kubadilishana pesa taslimu kibinafsi au kwenda benki.
WhatsApp imeunda kipengele chetu cha malipo kwa kushirikiana na Shirika la Malipo la India (NPCI) kwa kutumia Kiolesura Unganifu cha Malipo (UPI), mfumo wa malipo kwa muda halisi ambao ni wa kwanza nchini India, unaowezesha miamala na zaidi ya benki 160 zilizowezeshwa. Tunafurahi kujiunga na harakati za India za kuongeza urahisi na utumiaji wa malipo dijitali, hali inayosaidia kukuza ujumuishaji wa kifedha nchini India.
Ili kutuma pesa kwenye WhatsApp nchini India, ni muhimu uwe na akaunti ya benki na kadi ya malipo nchini India. WhatsApp hutuma maagizo kwa benki, ambazo pia zinajulikana kama watoa huduma za malipo, ili kuanzisha uhamishaji wa pesa kupitia UPI kati ya akaunti ya benki ya mtumaji na ya mpokeaji. Ni fahari yetu kufanya kazi na benki tano zinazoongoza nchini India: ICICI Bank, HDFC Bank, Axis Bank, Benki ya Taifa ya India, na Jio Payments Bank. Watu wanaweza kutuma pesa kwenye WhatsApp kwa yeyote anayetumia programu ya UPI iliyowezeshwa.
Baada ya muda, tunaamini muungano wa usanifu wa kipekee wa WhatsApp na UPI unaweza kusaidi mashirika ya ndani kutatua baadhi ya changamoto muhimu za wakati wetu, ikiwa ni pamoja na kuongeza ushiriki wa vijijini kwenye uchumi wa kidijitali na uwasilishaji wa huduma za kifedha kwa wale ambao hawajawahi kuwa nazo.
Kama ilivyo kwa kila kipengele kwenye WhatsApp, mfumo wa malipo umeundwa na viunzi imara vya usalama na kanuni za faragha, ikiwa ni pamoja na hitaji la kuweka PIN ya UPI kwa kila malipo. Malipo kwenye WhatsApp yanapatikana kwa watu walio na toleo la hivi karibuni la programu za iPhone na Android.
Kufikia leo, ujumbe wa WhatsApp hukaa daima kwenye simu zetu. Ingawa hali hiyo ni muhimu katika kudumisha kumbukumbu kutoka kwa familia na marafiki zetu, ujumbe mwingi tunaotuma haufai kudumu milele.
Lengo letu ni kufanya mazungumzo kwenye WhatsApp yahisi kama mazungumzo ya ana kwa ana kadri inavyowezekana, hii ina maana kwamba hayafai kubaki milele. Ndiyo maana tunafuraha kukuletea chaguo la ujumbe unaotoweka kwenye WhatsApp.
Hali ya ujumbe unaotoweka ikiwa imewashwa, ujumbe mpya unaotumwa kwenye soga utatoweka baada ya siku 7, hivyo kufanya mazungumzo yawe mepesi na ya faragha zaidi. Katika soga ya mtu na mwenzake, yeyote kati yao anaweza kuwasha au kuzima hali ya ujumbe unaotoweka. Katika vikundi, wasimamizi watakuwa na udhibiti.
Tunaanza kwa siku 7 kwa sababu tunafikiri kwamba itatoa utulivu wa akili ukijua kuwa mazungumzo hayatahifadhiwa milele, na pia yatadumu kwa muda wa kutosha hivi kwamba hutasahau soga ilihusu nini. Orodha ya bidhaa za kununua au anwani ya ilipo duka uliyopokea siku chache zilizopita itaendelea kuwa unapoihitaji, kisha itatoweka wakati huihitaji. Unaweza kusoma zaidi, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuwasha hali ya ujumbe unaotoweka hapa.
Tunataraji watu watafurahia hali ya ujumbe unaotoweka, hali hii itaanza kupatikana kwa watumiaji kila mahali mwezi huu.
Kwa miaka michache iliyopita, tumeona mabadiliko kwenye programu za utumaji ujumbe kwa mawasiliano ya kibinafsi na pia kwa ongezeko la watu wanaotegemea WhatsApp kwa kufanyia biashara zao.
Njia nyingi za zamani ambazo watu na biashara waliwasiliana nazo hazifanyi kazi. Ingawa biashara zinatumia mabilioni ya dola kila mwaka kugharimia mawasiliano ya simu, barua pepe na SMS, watu hawataki kusubiri simu zao zijibiwe, kupitishwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, au kukosa kujua kama ujumbe wao umepokelewa.
Janga la ulimwengu limeonyesha wazi kuwa biashara zinahitaji njia za haraka na za ufanisi za kuwahudumia wateja wao na kufanya mauzo. WhatsApp imekua rasilimali rahisi kwa wakati huu. Zaidi ya watu milioni 175 kila siku hutuma ujumbe kwenye akaunti ya WhatsApp Business. Utafiti wetu unaonyesha watu wanapendelea kutuma ujumbe kwa biashara ili kupata msaada na wana uwezekano mkubwa wa kununua wakati wanaweza kufanya hivyo.
Ingawa kuna mengi zaidi tunayohitaji kuunda. Kwa miaka miwili iliyopita, ili kusaidia tumetoa programu ya WhatsApp Business na API ya WhatsApp Business ili kusaidia biashara za ukubwa wote kudhibiti soga zao. Tumesikiliza maoni kuhusu yale yanayofanya kazi na tunaamini WhatsApp inaweza kusaidia kufanya utumaji ujumbe kuwa njia nzuri kwa watumiaji na biashara kuunganishwa. Ili kufikia hilo tunaongeza uwekezaji wetu kwenye maeneo yafuatayo:
Tunajua kuwa watu wengi wataendelea kutumia WhatsApp kwa mawasiliano na marafiki na familia, ikiwa ndiyo sababu tutaendelea kuunda vipengele vipya na kulinda mazungumzo ya watu ya kibinafsi.
Tunaamini maongezeko haya ya uzoefu kwenye WhatsApp yanakidhi mahitaji ya watu wengi na biashara kama wapo jirani au popote ulimwenguni. Kwa hakika yajayo yanapendeza na tutazindua hatua kwa hatua huduma hizi katika miezi ijayo.
WhatsApp inatoa lebo maalumu ya kusambaza kwenye ujumbe ulioshirikishwa kwa soga na ulisambazwa mara nyingi. Mishale hii miwili
Leo, tunaanzisha njia rahisi ya kuangalia mara mbili ujumbe huu kwa kugusa kitufe cha kioo cha kukuza kwenye soga. Kutoa njia rahisi ya kutafuta ujumbe ambao umesambazwa mara nyingi kunaweza kusaidia watu wengi kutafuta matokeo ya taarifa au vyanzo vingine vya habari kuhusu maudhui waliyopokea.
Kipengele hiki hufanya kazi kwa kuruhusu watumiaji kupakua ujumbe kupitia kwenye kivinjari bila WhatsApp kuuona ujumbe wenyewe.
Tafuta kwenye wavuti inazinduliwa kuanzia leo Brazil, Italia, Ireland, Meksiko, Uhispania, Uingereza na Marekani kwa wale wenye toleo la hivi karibuni la WhatsApp ya Android, iOS na WhatsApp Web.
Wakati biashara kote ulimwenguni zinajiandaa kufungua tena na kupanua mtandaoni, watu wanahitaji njia rahisi za kuwasiliana na biashara kuuliza maswali, kupata taarifa au kupata kitu ambacho wangependa kununua.
Leo tunaunga mkono zaidi ya watumiaji milioni 50 wa WhatsApp Business. Ili kuwasaidia hao na maelfu ya biashara kubwa kwenye API ya WhatsApp Business waweze kugundiliwa, tunaleta vipengele vipya ili kuanzisha soga na biashara kwenye WhatsApp na kuona ni bidhaa na huduma gani wanazotoa.
Kuanzisha soga na biashara kwa kutumia msimbo wa QR
Misimbo ya QR ni milango ya mbele ya kidijitali inayofanya kufungua kwa soga na biashara kuwa rahisii inavyowezekana. Awali watu walipokutana na biashara ya kuvutia, walihitaji kuongeza nambari yake ya WhatsApp kwenye anwani zao, nambari moja baada ya nyingine. Sasa, watu wanaweza kuchanganua msimbo wa QR unaonyeshwa mbele ya duka, kwenye furushi la bidhaa au risiti ili kuanzisha soga.
Kwa mfano, Ki Mindful Wearing, chapa inayotumika huko Brazil iliyotusaidia kujaribu kipengele hiki, inaweka msimbo wa QR kwenye vifurushi na vitambulisho vya bidhaa ili kuwaalika wateja kuomba msaada kwenye WhatsApp.
Kuchanganua msimbo wa QR kutafungua soga iliyo na ujumbe wa hiari wa awali ulioundwa na biashara ili kuanzisha mazungumzo. Pamoja na programu ya zana za utumaji ujumbe, biashara inaweza kutuma taarifa kwa haraka kama vile katalogi yao ili mazungumzo yaendelee. Kuanza kutumia msimbo wa QR, biashara zinaweza kufuata hatua hizi za haraka.
Misimbo ya QR yanapatikana kwa biashara kote duniani kwa kutumia programu ya WhatsApp Business au API ya WhatsApp Business kuanzia leo.
Kushiriki katalogi ili kugundua ni nini biashara inatoa
Katalogi inaruhusu biashara kuonyesha na kushiriki bidhaa au huduma wanazotoa, jambo ambalo linaweza kuwasaidia kukamilisha mauzo. Tangu kuzizindua mwaka uliopita, katalogi zimekuwa njia maarufu kwa watu kuhusiana na biashara kwenye WhatsApp. Kwa kweli, zaidi ya watu milioni 40 hutazama katalogi ya biashara kwenye WhatsApp kila mwezi.
Ili kufanya kuwe rahisi kwa watu kugundua bidhaa, tunafanya katalogi na vitu vya kibinafsi viweze kushirikishwa kama viungo kwenye tovuti, Facebook, Instagram na mahali pengine. Na kama watu wanataka kushirikisha katalogi au vitu wanavyovipata na marafiki wao au familia, wanaweza tu kunakili kiungo na kukituma kwenye WhatsApp au sehemu zingine pia.
Viungo vya katalogi vinapatikana ulimwenguni kote na biashara zinaweza kujifunza jinsi ya kuzishiriki hapa.
Ingawa barabara inayotangulia ya biashara itakuwa ndefu na yenye changamoto kadiri wanavyozoea hali mpya, tunatarajia kuwaunga mkono.