Tayari WhatsApp inatumiwa na kupendwa na watu zaidi ya bilioni 2 kote duniani. Wakati mwelekeo wetu unabakia kuwa njia rahisi, ya kuaminika na ya faragha kwa watu kupiga soga na marafiki na familia - sisi pia tunaendelea kusukuma mbele muundo wetu wa bidhaa ili kuhakikisha kuwa WhatsApp inabaki kuwa njia bora kwa mtu yeyote, mahali popote kujiunga.
Leo, tunafurahia kuthibitisha baadhi ya vipengele vipya ambavyo vinatolewa kwa muda wa wiki chache zijazo:
- Vibandiko Vilivyohuishwa: Vibandiko ni njia moja inayokua haraka ambayo watu wanawasiliana kwenye WhatsApp, na bilioni zikiwa zinatumwa kila siku. Tunatoa vifurushi vipya vya vibandiko vilivyohuishwa vitafurahisha zaidi na kujieleza zaidi.
- Misimbo ya QR: Tunafanya kuongeza mwasiliani mpya kuwa rahisi zaidi kuliko awali. Hivi karibuni utakapokutana na watu wapya, utaweza kukagua msimbo wao wa QR na kuwaongeza kwenye waasiliani wako. Hakuna tena kuandika tarakimu zao moja baada ya nyingine.
- Hali ya Giza ya WhatsApp Web na Desktop: Mandhari ya Hali ya Giza iliyo maarufu sana sasa inaenea kwa kompyuta yako.
- Uboreshaji wa simu za video za kikundi: Kwa sasa hadi watu 8 kwenye simu ya video, tumefanya kuwe rahisi kuzingatia mtu yeyote unayetaka kwa kukuruhusu ubonyeze na ushikilie kutanua video ya mshiriki ili iwe skrini kamilifu. Pia tumeongeza aikoni ya video kwenye soga za kikundi cha watu 8 au pungufu, ili uweze kuanzisha simu ya video ya kikundi kwa mguso 1.
- Hali inakuja kwa KaiOS: Watumiaji wa KaiOS wanaweza sasa kufurahia kipengele maarufu kinachoruhusu kushirikisha sasisho ambazo zinatoweka baada ya masaa 24.
Vipengele hivi vinatolewa kwa watumiaji kwa muda wa wiki chache zijazo, kwenye toleo la hivi karibuni la WhatsApp.