Tarehe 3 Aprili 2019
Vikundi vya WhatsApp vinaendelea kukuunganisha na familia, marafiki, wafanyakazi wenzako, wanafunzi wenzako, na zaidi. Vile watu wanavyotumia vikundi kwa mazungumzo muhimu, watumiaji wameomba udhibiti zaidi juu ya hali yao. Leo, tunaanzisha mipangilio ya faragha mpya na mfumo wa kukaribisha ili kukusaidia kuamua ni nani anayeweza kukuongeza kwenye vikundi.
Ili kuiwezesha, nenda kwenye Mipangilio katika programu yako, kisha uguse Akaunti > Faragha > Vikundi na uchague mojawapo ya chaguzi tatu: "Kila mtu," "Waasiliani Wangu," au "Waasiliani Wangu Isipokuwa." "Waasiliani Wangu" inamaanisha ni watumiaji ulio nao kwenye kitabu chako cha anwani pekee wanaoweza kukuweka kwenye vikundi na "Waasiliani Wangu Isipokuwa" hutoa udhibiti wa ziada wa ni nani kati ya watu unaowasiliana nao anayeweza kukuongeza kwenye kikundi.
Kwenye hali hizo, msimamizi ambaye hawezi kukuongeza kwenye kikundi atatakiwa kutuma mwaliko wa faragha kwa kupitia soga ya kibinafsi, kukupa hiari ya kujiunga na kikundi hicho. Utakuwa na siku tatu za kukubali mwaliko kabla ya muda wa mwaliko kuisha.
Kwa vipengele hivi vipya, watumiaji watakuwa na udhibiti zaidi wa jumbe za kikundi wanazopokea. Mipangilio hii mpya ya faragha itaanza kuwezeshwa kwa watumiaji wengine kuanzia leo na itakuwa inapatikana duniani kote katika siku zijazo kwa wale wanaotumia toleo la karibuni la WhatsApp.
SASISHA: Kulingana na maoni kutoka kwa watumiaji wakati wa uanzishaji wetu wa kwanza, badala ya chaguo la "Hakuna Mtu" sasa tunatoa chaguo la "Waasiliani Wangu Isipokuwa". Hii inakuwezesha kuchagua kutenganisha waasiliani maalum au "chagua wote". Sasisho hili linaanza kutumika kwa watumiaji duniani kote kwenye toleo la hivi karibuni la WhatsApp.
Ilisasishwa Mwisho: Tarehe 5 Novemba 2019