Aprili 3, 2019
Vikundi vya WhatsApp vinaendelea kukuunganisha na familia, marafiki, wafanyakazi wenzako, wanafunzi wenzako, na zaidi. Vile watu wanavyotumia vikundi kwa mazungumzo muhimu, watumiaji wameomba udhibiti zaidi juu ya uzoefu wao. Leo, tunatambulisha mpangilio wa faragha mpya na mfumo wa kualika ili kukusaidia kuamua ni nani anayeweza kukuongeza kwenye vikundi.
Kuiwezesha, nenda kwenye Mipangilio ya programu yako, kisha gusa Akaunti > Faragha > Vikundi na chagua mojawapo ya hiari tatu: “Kila Mtu,” “Waasiliani Wangu,” au “Waasiliani Wangu Isipokua.” “Waasiliani Wangu” inamaanisha kuwa watumiaji tu waliopo kwenye kitabu chako cha anwani ndiyo wanaoweza kukuongeza kwenye vikundi na “Waasiliani Wangu Isipokuwa” hutoa udhibiti wa ziada kwa nani miongoni mwa waasiliani wako wanaweza kukuongeza kwenye kikundi.
Kwenye kesi hizo, mtawala ambaye hawezi kukuongeza kwenye kikundi atatakiwa kutuma mwaliko wa faragha kwa kupitia soga ya kibinafsi, kukupa hiari ya kujiunga na kikundi hicho. Utakuwa na siku tatu za kukubali mwaliko kabla ya muda wake kuisha.
Kwa vipengele hivi vipya, watumiaji watakuwa na udhibiti zaidi wa jumbe za kikundi wanazopokea. Mipangilio hii mpya ya faragha itaanza kuwezeshwa kwa watumiaji wengine kuanzia leo na itakuwa inapatikana duniani kote katika siku zijazo kwa wale wanaotumia toleo la karibuni la WhatsApp.
SASISHO: Kulingana na maoni kutoka kwa watumiaji wakati wa usambazaji wetu wa awali, badala ya chaguo la "Hakuna mtu" sasa tunatoa hiari ya “Waasiliani Wangu Isipokuwa”. Hii inakuwezesha kuchagua kutenganisha waasiliani maalum au "chagua wote". Sasisho hili linasambaziwa kwa watumiaji duniani kote kwenye toleo la hivi karibuni la WhatsApp.
Mwisho Ilisasishwa: Novemba 5, 2019