Nenda kwenye maudhui
  • Nyumbani
    • Tuma ujumbe faraghaniKaa mtandaoniJenga jumuiyaJielezeWhatsApp ya biashara
  • Faragha
  • Kituo cha Msaada
  • Blogu
  • Kwa Biashara
  • Pakua
Pakua
Sheria na Sera ya Faragha2023 © WhatsApp LLC
Ukurasa Mkuu wa WhatsAppUkurasa Mkuu wa WhatsApp
    • Tuma ujumbe faraghani

      Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho na vidhibiti vya faragha.

    • Kaa mtandaoni

      Tuma ujumbe na upige simu bila malipo* kote ulimwenguni.

    • Jenga jumuiya

      Mazungumzo ya vikundi yamerahisishwa.

    • Jieleze

      Jieleze kwa vibandiko, GIF, Picha na zaidi.

    • Biashara ya WhatsApp

      Fikia wateja wako popote walipo.

  • Faragha
  • Kituo cha Msaada
  • Blogu
  • Kwa Biashara
  • WhatsApp Web
  • Pakua
Pakua
Rudi kwenye Blogu
Blogu ya WhatsApp

Njia Mpya za kufikia Biashara kwenye WhatsApp

Wakati biashara kote ulimwenguni zinajiandaa kufungua tena na kupanua mtandaoni, watu wanahitaji njia rahisi za kuwasiliana na biashara kuuliza maswali, kupata taarifa au kupata kitu ambacho wangependa kununua.

Leo tunaunga mkono zaidi ya watumiaji milioni 50 wa WhatsApp Business. Ili kuwasaidia hao na maelfu ya biashara kubwa kwenye API ya WhatsApp Business waweze kugunduliwa, tunaleta vipengele vipya ili kuanzisha soga na biashara kwenye WhatsApp na kuona ni bidhaa na huduma gani wanazotoa.

Kuanzisha soga na biashara kwa kutumia misimbo ya QR

Misimbo ya QR ni njia rahisi kidijitali inayofanya kufungua kwa soga na biashara kuwa rahisi inavyowezekana. Awali watu walipokutana na biashara ya kuvutia, walihitaji kuongeza nambari yake ya WhatsApp kwenye anwani zao, nambari moja baada ya nyingine. Sasa, watu wanaweza kuchanganua msimbo wa QR unaonyeshwa mbele ya duka, kwenye furushi la bidhaa au risiti ili kuanzisha soga.

Kwa mfano, Ki Mindful Wearing, chapa inayotumika huko Brazil iliyotusaidia kujaribu kipengele hiki, inaweka msimbo wa QR kwenye vifurushi na vitambulisho vya bidhaa ili kuwaalika wateja kuomba msaada kwenye WhatsApp.

Kuchanganua msimbo wa QR kutafungua soga iliyo na ujumbe wa hiari wa awali ulioundwa na biashara ili kuanzisha mazungumzo. Pamoja na programu ya zana za utumaji ujumbe, biashara inaweza kutuma taarifa kwa haraka kama vile katalogi yao ili mazungumzo yaendelee. Ili zianze kutumia msimbo wa QR, biashara zinaweza kufuata hatua hizi za haraka.

Misimbo ya QR inapatikana kwa biashara kote duniani kwa kutumia programu ya WhatsApp Business au API ya WhatsApp Business kuanzia leo.

Kushirikisha katalogi ili kugundua vitu vinavyotolewa na biashara

Katalogi inaruhusu biashara kuonyesha na kushiriki bidhaa au huduma wanazotoa, jambo ambalo linaweza kuwasaidia kufanya mauzo. Tangu kuzizindua mwaka uliopita, katalogi zimekuwa njia maarufu kwa watu kuhusiana na biashara kwenye WhatsApp. Kwa kweli, zaidi ya watu milioni 40 hutazama katalogi ya biashara kwenye WhatsApp kila mwezi.

Ili kufanya kuwe rahisi kwa watu kugundua bidhaa, tunafanya katalogi na vitu vya kibinafsi viweze kushirikishwa kama viungo kwenye tovuti, Facebook, Instagram na mahali pengine. Na kama watu wanataka kushirikisha katalogi au vitu wanavyovipata na marafiki wao au familia, wanaweza tu kunakili kiungo na kukituma kwenye WhatsApp au sehemu zingine pia.

Viungo vya katalogi vinapatikana duniani kote na biashara zinaweza kujifunza jinsi ya kuvishiriki hapa.

Ingawa mustakabali wa biashara utakuwa mrefu na wenye changamoto kadiri wanavyozoea hali mpya, tunatarajia kuwapa usaidizi.

Julai 9, 2020

Pakua
Nembo Kuu ya WhatsApp
Nembo Kuu ya WhatsApp
Pakua
Huduma ZetuVipengeleBloguUsalamaKwa Biashara
Sisi ni naniKutuhusu sisiKaziKituo cha ChapaFaragha
Tumia WhatsAppAndroidiPhoneMac/PCWhatsApp Web
Unahitaji msaada?Wasiliana NasiKituo cha MsaadaPakuaUshauri wa Usalama
Pakua

WhatsApp LLC 2023 ©

Sheria na Sera ya Faragha