Nenda kwenye maudhui
  • Nyumbani
    • Tuma ujumbe faraghaniUsiachwe nyumaJenga jumuiyaJielezeWhatsApp ya biashara
  • Faragha
  • Kituo cha Msaada
  • Blogu
  • Kwa Biashara
Pakua
Sheria na Sera ya Faragha2023 © WhatsApp LLC
Ukurasa Mkuu wa WhatsAppUkurasa Mkuu wa WhatsApp
    • Tuma ujumbe faraghani

      Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho na vidhibiti vya faragha.

    • Usiachwe nyuma

      Tuma ujumbe na upige simu bila malipo* kote ulimwenguni.

    • Jenga jumuiya

      Mazungumzo ya vikundi yamerahisishwa.

    • Jieleze

      Jieleze kwa vibandiko, GIF, Picha na zaidi.

    • Biashara ya WhatsApp

      Fikia wateja wako popote walipo.

  • Faragha
  • Kituo cha Msaada
  • Blogu
  • Kwa Biashara
WhatsApp WebPakua
Blogu ya WhatsApp

Ununuzi, Malipo na Huduma kwa Mteja kwenye WhatsApp

Kwa miaka michache iliyopita, tumeona mabadiliko kwenye programu za utumaji ujumbe kwa mawasiliano ya kibinafsi na pia kwa ongezeko la watu wanaotegemea WhatsApp kwa kufanyia biashara zao.

Njia nyingi za zamani ambazo watu na biashara waliwasiliana nazo hazifanyi kazi. Ingawa biashara zinatumia mabilioni ya dola kila mwaka kugharimia mawasiliano ya simu, barua pepe na SMS, watu hawataki kusubiri simu zao zijibiwe, kupitishwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, au kukosa kujua kama ujumbe wao umepokelewa.

Janga la ulimwengu limeonyesha wazi kuwa biashara zinahitaji njia za haraka na za ufanisi za kuwahudumia wateja wao na kufanya mauzo. WhatsApp imekua rasilimali rahisi kwa wakati huu. Zaidi ya watu milioni 175 kila siku hutuma ujumbe kwenye akaunti ya WhatsApp Business. Utafiti wetu unaonyesha watu wanapendelea kutuma ujumbe kwa biashara ili kupata msaada na wana uwezekano mkubwa wa kununua wakati wanaweza kufanya hivyo.

Ingawa kuna mengi zaidi tunayohitaji kuunda. Kwa miaka miwili iliyopita, ili kusaidia tumetoa programu ya WhatsApp Business na API ya WhatsApp Business ili kusaidia biashara za ukubwa wote kudhibiti soga zao. Tumesikiliza maoni kuhusu yale yanayofanya kazi na tunaamini WhatsApp inaweza kusaidia kufanya utumaji ujumbe kuwa njia nzuri kwa watumiaji na biashara kuunganishwa. Ili kufikia hilo tunaongeza uwekezaji wetu kwenye maeneo yafuatayo:

  • Ununuzi - Tutapanua njia za watu kuangalia bidhaa zilizopo na kufanya ununuzi kutoka hapohapo kwenye soga. Pia tunataka kufanya kuwe rahisi kwa biashara kujumuisha vipengele hivi kwenye suluhisho walizonazo za kibiashara na wateja. Hii itasaidia biashara nyingi ndogo ambazo zimeathiriwa zaidi wakati huu.
  • Huduma za Upangishaji za Facebook - Biashara zina mahitaji tofauti ya kitekinolojia na zinahitaji kuchagua kampuni za kufanya kazi nazo kupangisha na kudhibiti mawasiliano ya wateja, hasa kwa ajili la ongezeko la kufanya kazi kwa mbali. Ndiyo sababu zaidi ya miezi ijayo, tunapanga kupanua ushirikiano wetu na watoaji suluhisho ya biashara ambao tumefanya kazi nao kwa miaka miwili iliyopita. Pia tutatoa hiari mpya kwa biashara kusimamia ujumbe wao wa WhatsApp kupitia huduma za upangishaji ambazo Facebook inapanga kutoa. Kutoa hiari kutafanya rahisi kwa biashara ndogo na ukubwa wa wastani kuanza, kuuza bidhaa, kutunza kitabu cha orodha ya vitu, kujibu ujumbe wanaopokea kwa haraka - popote pale waajiriwa wao walipo.
  • Mauzo ya Biashara - Tutatoza wateja wa biashara kwa baadhi ya huduma tunazotoa, hatua itakayosaidia WhatsApp kuendelea kujenga biashara yetu wenyewe huku tukitoa na kukuza huduma za ujumbe wa maandishi, simu za video na za sauti, zote zilizo na ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, bure kwa zaidi ya watu bilioni mbili.

Tunajua kuwa watu wengi wataendelea kutumia WhatsApp kwa mawasiliano na marafiki na familia, ikiwa ndiyo sababu tutaendelea kuunda vipengele vipya na kulinda mazungumzo ya watu ya kibinafsi.

Tunaamini maongezeko haya ya uzoefu kwenye WhatsApp yanakidhi mahitaji ya watu wengi na biashara kama wapo jirani au popote ulimwenguni. Kwa hakika yajayo yanapendeza na tutazindua hatua kwa hatua huduma hizi katika miezi ijayo.

Oktoba 22, 2020

TweetShiriki
Pakua
Nembo Kuu ya WhatsApp
Nembo Kuu ya WhatsAppPakua
Huduma ZetuVipengeleBloguUsalamaKwa Biashara
Sisi ni naniKutuhusuKaziKituo cha ChapaFaragha
Tumia WhatsAppAndroidiPhoneMac/PCWhatsApp Web
Unahitaji msaada?Wasiliana nasiKituo cha MsaadaVirusi vya KoronaUshauri wa Usalama
Pakua

WhatsApp LLC 2023 ©

Sheria na Sera ya Faragha