Tarehe 2 Septemba, 2021
Sasa unaweza pia kuhamisha soga zako zote za WhatsApp kutoka Android hadi iPhone unapobadilisha simu.
Ni wewe unayemiliki ujumbe wako kwenye WhatsApp. Ndiyo maana ujumbe wako binafsi kwenye WhatsApp hulindwa kupitia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho na ndiyo maana tuna chaguo za kufanya ujumbe utoweke kiotomatiki kwenye soga zako.
Mojawapo ya vipengele ambavyo vimependekezwa sana ni kuwawezesha watumiaji kuhamisha soga kutoka mfumo mmoja wa uendeshaji hadi mwingine wanapobadilisha simu. Tumefanya jitihada kwa ushirikiano na watengenezaji wa vifaa na mifumo ya uendeshaji ili kusanidi kipengele hiki kwa njia salama na thabiti.
Tunafuraha kuzindua kipengele hiki kinachokuwezesha kuhamisha soga zako za WhatsApp kutoka iOS hadi Android. Hili hufanyika bila ujumbe wako kutumwa kwa WhatsApp na pia inajumuisha ujumbe wa sauti, picha na video. Kipengele hiki kinapatikana kwa vifaa vinavyotumia Android 12 na matoleo mapya zaidi.
Unapoweka mipangilio kwenye kifaa kipya, utapewa chaguo la kuhamisha soga zako kwa njia salama kutoka kwenye kifaa ulichokuwa ukitumia hadi kwenye kifaa kipya. Unahitaji kebo ya USB-C ambayo upande mmoja unaunganisha vifaa vya Apple (Lightning). Maelezo zaidi yanapatikana kwenye here.
Huu ni mwanzo tu. Tunatazamia kutoa kipengele hiki kwa watumiaji zaidi ili kuwawezesha kuhamia kwenye mifumo wanayopenda na kuhamisha soga zao kwa njia salama.
Mara ya Mwisho Kusasishwa: Julai 20, 2022