Februari 12, 2020
Tumefurahi kuwaeleza kwamba, kama ya leo, WhatsApp inasaidia zaidi ya watumiaji bilioni mbili duniani kote.
Akina mama na akina baba wanaweza kuwapata wapendwa wao popote walipo. Akina kaka na dada wanaweza kushirikisha muda muhimu. Wafanyakazi wanaweza kushirikiana, na biashara inaweza kukua kwa kuunganisha kirahisi na wateja wao.
Mazungumzo ya kibinafsi ambayo wakati mmoja yaliwezekana tu kwa ana-kwa-ana sasa zinaweza kufanyika katika umbali mkubwa kupitia soga za papo hapo na simu ya video. Kuna wakati mwingi muhimu na maalum ambayo yanafanyika kwenye WhatsApp na tunajinyenyekea na kupokea heshima ya kufikia hatua hii kuu.
Tunajua kwamba tunavyoungana zaidi, ndvyo tunavyohitaji kulinda zaidi. Tunapoendesha zaidi maisha yetu mtandaoni, kulinda mazungumzo yetu ni muhimu zaidi kuliko hapo awali.
Ndiyo sababu kila ujumbe wa kibinafsi uliotumwa kwa kutumia WhatsApp umelindwa kimsingi na ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho. Ufumbaji imara ni kama kufuli ya kidijitali ambacho hakiwezi kuvunjwa na kinaweka maelezo unayotuma kwa kupitia WhatsApp salama, kukusaidia kukulinda kutoka kwa wadadisi na wahalifu. Ujumbe huhifadhiwa tu kwenye simu yako, na hakuna mtu kati anayeweza kusoma ujumbe wako au kusikiliza simu zako, hata sisi. Mazungumzo yako ya kibinafsi yanakaa kati yenu.
Ufumbaji imara ni jambo la lazima katika maisha ya kisasa. Hatutakiuka juu ya usalama kwa sababu kufanya hivyo kutafanya watu kupungukiwa kidogo na usalama. Ili kuwa na usalama zaidi, tunafanya kazi na wataalam wa hali ya juu wa usalama, kutumia teknolojia inayoongoza kusimamisha matumizi mabaya na vile vile kutoa udhibiti na njia za kuripoti maswala — bila kupunguza faragha.
WhatsApp ilianza na lengo la kuunda huduma ambayo ni rahisi, ya kuaminika, na ya faragha kwa watu kutumia. Leo tunabaki tumejitolea kama vile tulipoanza, kusaidia kuunganisha ulimwengu kifaragha na kulinda mawasiliano ya kibinafsi ya watumiaji bilioni mbili ulimwenguni.