Nenda kwenye maudhui
  • Nyumbani
    • Tuma ujumbe faraghaniKaa mtandaoniJenga jumuiyaJielezeWhatsApp ya biashara
  • Faragha
  • Kituo cha Msaada
  • Blogu
Pakua
Masharti ya Huduma2023 © WhatsApp LLC
Ukurasa Mkuu wa WhatsAppUkurasa Mkuu wa WhatsApp
    • Tuma Ujumbe Faraghani

      Ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho na vidhibiti vya faragha.

    • Kaa mtandaoni

      Fikia wateja wako ulimwenguni.

    • Jenga jumuiya

      Mazungumzo ya kikundi yamerahisishwa.

    • Jieleze

      Jieleze kwa vibandiko, GIF, Picha na zaidi.

    • WhatsApp Business

      Fikia wateja wako popote walipo.

  • Faragha
  • Kituo cha Msaada
  • Blogu
WhatsApp WebPakua
Blogu ya WhatsApp

Kuwezesha Biashara Zote Kuendesha Shughuli zao kwenye WhatsApp kwa Urahisi

Kwa watu na biashara kote ulimwenguni, shughuli za kibiashara sasa zinafanyika kwenye WhatsApp. Iwe ni duka la rejareja au kampuni lililoorodheshwa kwenye jarida la Fortune 500, biashara kubwa na ndogo leo zinategemea WhatsApp katika kuwahudumia wateja wao.

Kama ambavyo WhatsApp imewezesha wapendwa kuwasiliana kwa urahisi wakiwa mbali, tungependa kushughulikia changamoto ambazo sote tumepitia tunapohitaji kuwasiliana na wafanyabiashara. Hii inamaanisha hakuna tena kusubiri muda mrefu, kukumbwa na hitilafu kwenye tovuti isiyofanya kazi, au kutuma barua pepe bila uhakika kuwa itasomwa.

Kufikia sasa, tumesaidia kuboresha mamilioni ya biashara kwa kutumia WhatsApp. Hatua inayofuata ni kutoa huduma ya WhatsApp kwa kila biashara inayohitaji kuwasiliana na wateja wake kwa njia rahisi, ya haraka na ya kutegemewa.

Kutoa WhatsApp kwa Biashara na Wasanidi Wote kwa kutumia API Mpya ya Wingu

Leo tunachukua hatua muhimu katika kutoa huduma ya WhatsApp kwa biashara kubwa na ndogo kote ulimwenguni kupitia huduma salama zisizolipishwa za kupangisha programu kwenye wingu zinazotolewa na Meta. Kwa kutumia API hii mpya, tumepunguza muda wa kusubiri usajili kutoka miezi kadhaa hadi dakika chache ili biashara na wasanidi waweze kufikia huduma yetu haraka na kwa urahisi, kutumia mfumo wa WhatsApp ambao tayari upo ili kubadilisha hali ya utumiaji kuwafaa na kuweza kuwasiliana na wateja wao kwa haraka zaidi. Huduma hizi pia zitaondolea washirika wetu gharama kubwa za seva na zitawawezesha kufikia vipengele vipya papo hapo. Biashara zinaweza kujisajili moja kwa moja au kushirikiana na mmoja wa watoa huduma zetu za biashara ili kuanza.

Programu ya WhatsApp Business ina Vipengele Vipya Vinavyofaa Biashara Zinazokua Haraka

Kwa miaka kadhaa sasa tumeona jinsi biashara ndogo ndogo zinazotumia WhatsApp zimekua, hivyo tungependa kutoa zana za ziada ili biashara hizi ziendelee kunawiri. Tunatarajia kuwa baadhi ya biashara zitapendelea kutumia API ya Wingu japo biashara nyingi zitaendelea kutumia programu ya WhatsApp Business. Pia tunasanidi vipengele vya kina vitakavyotumiwa na biashara hizi ili kuzisaidia kufikia wateja wengi na kujitangaza mtandaoni – kama vile uwezo wa kudhibiti soga kwenye hadi vifaa 10 ili kuziwezesha kushughulikia vyema soga nyingi. Pia tutatoa viungo vipya unavyoweza kubadilisha na vinavyokuwezesha kupiga soga kwenye WhatsApp unapobofya, ili kusaidia biashara kuvutia wateja kote mtandaoni. Tunapanga vyote hivi viwe vipengele vya ziada, vya kuchagua na vinavyolipishwa kwenye programu ya WhatsApp Business kama sehemu ya huduma mpya inayolipishwa. Tutashiriki maelezo zaidi baadaye.

Njia hizi mpya za kusaidia biashara haziathiri maadili yetu kuhusiana na mazungumzo kati ya mtu na biashara. Wewe ndiye unadhibiti soga kati yako na biashara na hutapokea ujumbe kutoka kwa biashara ikiwa hujawaomba wawasiliane nawe.

Tunatumai watu watafurahia kupiga soga na biashara wanazozipenda kwenye WhatsApp, na ni matarajio yetu kuwa biashara mpya zitachipuka, zitajikuza na zitastawi.

19 Mei, 2022

TweetShiriki

Emoji za kuonyesha hisia, Kushiriki Faili za GB 2, Vikundi vya 512

Emoji za kuonyesha hisia kwenye WhatsApp zimeboreshwa zaidi kupitia kibodi nzima ya emoji inayojumuisha chaguo la rangi ya ngozi. Tunafuraha kuwaletea watumiaji chaguo zaidi wanazoweza kutumia kujieleza wanapopiga soga na familia na marafiki.

Kama tulivyotangaza mwezi uliopita maono yetu kuhusu Jumuiya kwenye WhatsApp, sasa mashirika, biashara, na vikundi vya watu wanaotangamana kwa ukaribu wanaweza kuwasiliana kwa njia salama na kutekeleza mambo wanayolenga kwenye WhatsApp. Maoni ambayo tumepokea kufikia sasa yamekuwa mazuri sana na tunatazamia kutoa vipengele vingi vipya kwa watumiaji.

Tunafuraha kutangaza kuwa emoji za kuonyesha hisia sasa zinapatikana kwenye toleo jipya zaidi la programu. Emoji hizi zinafurahisha, ni rahisi kutumia na zinapunguza soga katika vikundi. Tutaendelea kuziboresha kwa kuongeza emoji zaidi katika siku zijazo.

Pia, sasa unaweza kutuma faili za hadi GB 2 zilizolindwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye WhatsApp. Ukubwa huu umeongezwa kutoka kikomo cha awali cha MB 100 na tunaamini kuwa hili litawezesha ushirikiano kati ya biashara ndogo ndogo na vikundi vya shule. Tunapendekeza utumie WiFi kwa faili kubwa na utaona kipima muda unapopakia au kupakua ili ujue muda ambao uhamishaji wako utachukua.

Mojawapo ya maombi muhimu ambayo tumepokea mara nyingi ni chaguo la kuongeza watu zaidi kwenye soga. Kwa sasa tumeanza kwa kuwezesha hadi watu 512 kuongezwa kwenye kikundi. Kudumisha jumuiya binafsi, salama na za faragha kunahusisha majukumu mengi na tunaamini kuwa maboresha haya yatawezesha watu na vikundi kutangamana kwa ukaribu.

Tunatumai watu watafurahia masasisho haya na tunatarajia kutoa maboresho zaidi mwaka mzima.

Mara ya Mwisho Kusasishwa: tarehe 11 Julai, 2022

Mei 5, 2022

TweetShiriki

Kushiriki Maono Yetu kuhusu Jumuiya kwenye WhatsApp

Leo tuna furaha kushiriki maono yetu kuhusu kipengele kipya tunachoongeza kwenye WhatsApp kinachojulikana kama Jumuiya. Tangu tulipozindua WhatsApp mwaka wa 2009, lengo letu limekuwa kuwasaidia watu kuwasiliana kwa njia inayokaribiana na mazungumzo ya ana kwa ana wanapotaka kuzungumza na mtu binafsi, kikundi cha marafiki au familia. Pia, mara kwa mara tunapokea maoni kutoka kwa watu wanaotumia WhatsApp kuwasiliana na kuratibu shughuli katika jumuiya.

Mashirika kama vile shule, vikundi vya kieneo na mashirika yasiyo ya faida sasa yanatumia WhatsApp kuwasiliana kwa njia salama na kutekeleza mambo — hasa baada ya janga kutuchochea kutafuta njia za ubunifu za kufanya kazi pamoja tukiwa sehemu mbalimbali. Kutokana na maoni mengi ambayo tumepokea, tunaamini kuwa kuna mengi tunayoweza kufanya ili kuwawezesha watu kudhibiti mazungumzo haya yanayofanyika sana katika vikundi hivi.

Yote haya yatawezekana kupitia kipengele cha Jumuiya. Jumuiya kwenye WhatsApp zitawawezesha watu kuleta pamoja vikundi tofauti katika jumuiya moja inayowafaa. Kupitia hili, watu wanaweza kupokea taarifa zinazotumwa kwenye Jumuiya nzima na kupanga kwa urahisi vikundi vidogo vya kujadiliana kuhusu yaliyo muhimu kwao. Jumuiya pia zitajumuisha zana mpya mahiri kwa wasimamizi, ikiwemo kudhibiti vikundi vinavyoweza kujumuishwa, na ujumbe wa kutaarifu unaotumwa kwa watu wote.

Tunaamini kuwa Jumuiya zitamwezesha mwalimu mkuu wa shule kuwaleta pamoja wazazi wote wa shule ili kushiriki nao habari muhimu na kuanzisha vikundi vya madarasa mbalimbali, shughuli za ziada, au uhisani.

Pia tunafanya maboresho kadhaa kuhusu jinsi vikundi hufanya kazi kwenye WhatsApp — iwe vikundi hivyo ni sehemu ya Jumuiya au la. Tunaamini maboresho haya yatasaidia watu kushiriki maudhui kwa njia mpya na yatapunguza upakiaji wa soga nyingi mno katika vikundi vyenye washiriki wengi. Vipengele hivi vitapatikana katika wiki zijazo ili watu waanze kuvijaribu hata kabla ya Jumuiya kuwa tayari.

  • Maoni - Kipengele cha maoni ya emoji kitazinduliwa kwenye WhatsApp ili watu waweze kushiriki maoni yao kwa haraka bila kutuma ujumbe mpya kwenye soga.
  • Idhini ya Wasimamizi Kufuta Ujumbe - Wasimamizi wa vikundi wataweza kuondoa ujumbe usioruhusiwa au usiokubalika kwenye soga ya kila mtu.
  • Kushiriki Faili – Tunaongeza ukubwa wa faili unayoweza kushiriki hadi gigabaiti 2 ili watu waweze kushirikiana kwa urahisi katika miradi.
  • Simu za Kikundi Kikubwa – Tutazindua kipengele cha simu ya sauti chenye muundo mpya kinachoruhusu kupiga simu kwa hadi watu 32 kwa kugusa mara moja, wakati ambapo kuzungumza moja kwa moja kutafaa kuliko kupiga soga.

Mawasiliano kwenye jumuiya ni ya faragha, ndio maana tutaendelea kulinda ujumbe kupitia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho. Teknolojia hii ya usalama ni muhimu sana katika kulinda faragha na usalama wa watu. Vikundi vya watu wanaoshirikiana kwa ukaribu — shule, washirika wa kanisa, hata wafanyabiashara — wangependa na wanahitaji kuwa na mazungumzo salama na ya faragha bila WhatsApp kufuatilia kila wanachokifanya. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyoshughulikia faragha, usalama na ulinzi wa jumuiya hapa.

Ingawa programu zingine zinabuni njia za kupiga soga kwa ajili ya mamia ya maelfu ya watu, tunalenga kusaidia vikundi ambavyo ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Jumuiya kwenye WhatsApp ni huduma mpya hivyo lengo letu katika kipindi cha mwaka moja ujao ni kubuni vipengele vipya vitakavyotumika. Tunafuraha kuwaletea watumiaji huduma ya Jumuiya na tunatazamia kupokea maoni yao.

Aprili 14, 2022

TweetShiriki

Tumeboresha Huduma ya Ujumbe wa Sauti

Tulipozindua huduma ya ujumbe wa sauti kwa mara ya kwanza mwaka wa 2013, tulijua kuwa itabadilisha jinsi watu wanavyowasiliana. Kwa kutumia muundo rahisi, tumefanya kurekodi na kutuma ujumbe wa sauti kuwa haraka na rahisi kama kuandika ujumbe. Kwa wastani, watumiaji wetu hutuma jumbe za sauti bilioni 7 kila siku kwenye WhatsApp, na jumbe hizi zote zinalindwa kupitia usimbaji fiche wa mwisho hadi mwisho ili kudumisha faragha na usalama wake kila wakati.

Tunafuraha leo kutangaza vipengele vipya vinavyoboresha utumaji wa ujumbe wa sauti kwenye WhatsApp. Vipengele hivi vinajumuisha:

  • Kucheza Ujumbe Nje ya Gumzo: Sikiliza ujumbe wa sauti nje ya gumzo ili uweze kusoma na kujibu ujumbe mwingine au kutekeleza shughuli kadhaa kwa wakati mmoja.
  • Kusitisha au Kuendelea Kurekodi Ujumbe: Unaporekodi ujumbe wa sauti, sasa unaweza kusitisha kurekodi kisha uendelee ukiwa tayari, ikiwa utakatizwa au unahitaji kuwazia jambo fulani kwanza.
  • Mawimbi ya Uchezaji wa Ujumbe: Yanaonyesha mtiririko wa sauti kwenye ujumbe wa sauti ili kukusaidia kufuatilia rekodi.
  • Kusikiliza Ujumbe Kabla ya Kuutuma: Sikiliza ujumbe wako wa sauti kabla ya kuutuma.
  • Kukumbuka Ujumbe wa Sauti Uliocheza: Unaposikiliza ujumbe wa sauti kisha usitishe, unaweza kuendelea ulipoachia utakaporejea kwenye gumzo.
  • Cheza Haraka Ujumbe Uliosambazwa: Cheza ujumbe wa sauti kwa kasi ya 1.5x au 2x ili usikilize haraka ujumbe wa kawaida na ule uliosambazwa.

Ujumbe wa sauti umewawezesha watu kujieleza vyema zaidi kwa urahisi na haraka. Kuonyesha hisia au msisimko ukitumia maneno ni rahisi zaidi kuliko maandishi, na katika hali nyingi, ujumbe wa sauti ndiyo njia inayopendelewa ya mawasiliano kwenye WhatsApp. Ni rahisi kwa mtu yeyote kutumia - kwa wanafamilia wasiopendelea kuandika ujumbe, kwa marafiki wanaopenda kusimulia hadithi, kwa wenzako wanaohitaji kutiwa moyo, au unapotaka kusikia sauti ya mpendwa wako mwishoni mwa siku ndefu yenye uchovu.

Tunasubiri kwa hamu kuona wateja wetu wakijaribu vipengele hivi vipya vitakapotolewa katika wiki zijazo.

Machi 30, 2022

TweetShiriki

Udhibiti na Faragha zaidi kutokana na Ujumbe unaotoweka kwa Chaguomsingi na Vipindi Tofauti vya Muda

Lengo letu ni kufanikisha mawasiliano duniani kwa faragha. Huku mawasiliano yetu mengi yakizidi kuhamia mifumo ya dijitali kutoka ana kwa ana, tunatambua kwamba kuna upekee fulani wa kuketi na mtu na kushauriana naye uso kwa macho, mkielezana mawazo yenu kwa ujasiri, mkifahamu kwamba mnawasiliana kwa faragha na kwa wakati halisi. Uhuru wa kusema ukweli na kufungua roho, huku mkijua kwamba mazungumzo yenu hayanakiliwi na kuhifadhiwa mahali fulani milele.

Basi unafaa kuwa na uhuru wa kuamua ujumbe wako utadumu kwa muda gani. Tumezoea kuacha nakala dijitali ya karibu kila kitu tunachoandika hata bila kufikiria. Imekuwa kama daftari linaloandamana nasi kila mahali na kuunda rekodi ya kudumu ya kila kitu tunachosema. Hii ndiyo maana mwaka uliopita tulizindua ujumbe unaotoweka na hivi karibuni, tumeanzisha kipengele cha picha na video zinazotoweka pindi tu baada ya kuzitazama mara moja.

Leo tunafuraha ya kuwawezesha watumiaji wetu kuwa na udhibiti zaidi juu ya ujumbe wao na muda ambao ujumbe unadumu. Tuna vipengele vya kuwezesha ujumbe kutoweka kwa chaguomsingi, hali kadhalika vipindi tofauti vya muda ambao ujumbe unaweza kudumu.

Watumiaji wa WhatsApp sasa watakuwa na chaguo la kuwasha ujumbe unaotoweka kwenye soga zao zote mpya. Hali hii ikiwashwa, ujumbe wote mpya unaoanzisha ili kuwasiliana na mtu mwingine au ambao mtu anaanzisha ili kuwasiliana na wewe utatoweka baada ya muda uliochagua. Pia tumeongeza chaguo jipya wakati unaanzisha soga ya kikundi linalokuwezesha kuwasha hali hii unapoanzisha kikundi kipya. Kipengele hiki kipya ni cha hiari na hakibadili wala kufuta soga zako zozote zilizopo.

Pia tunaongeza chaguo mbili za muda ambao ujumbe unaotoweka utadumu: Saa 24 na siku 90, pamoja na chaguo lililopo la siku 7.

Kwa watu wanaochagua kuwasha hali ya ujumbe kutoweka kwa chaguomsingi, tunaonyesha ujumbe kwenye soga zako ili kuwajulisha watu muda chaguomsingi uliouchagua. Ujumbe huo hubainisha wazi kwamba si uamuzi unaomlenga mtu mmoja, bali ni chaguo la jinsi unavyotaka kuwasiliana na kila mtu kwenye WhatsApp kuanzia sasa kwenda mbele. Hata hivyo, kama ungependa ujumbe fulani udumu, ni rahisi kubadilisha.

Kutokuwa karibu na ndugu na marafiki kwa zaidi ya mwaka mmoja kumetudhihirishia wazi kwamba ingawa hatuwezi kuzungumza ana kwa ana, haimaanishi kwamba tunafaa kutojali faragha ya mawasiliano yetu ya binafsi. Tunaamini kuwa ujumbe unaotoweka pamoja na ufumbaji wa mwisho hadi mwisho ni vipengele viwili muhimu vinavyohimili jinsi ya kuwasiliana kwa faragha katika zama hizi. Vipengele hivi vinatuleta karibu na kupata hali sawa na mazungumzo ya ana kwa ana.

Ili uanze, nenda katika mipangilio ya Faragha kisha uchague ‘Muda Chaguomsingi wa Ujumbe’. Unaweza kupata maelezo zaidi hapa.

Tarehe 6 Desemba, 2021

TweetShiriki

Nakala za Soga Zilizofumbwa Mwisho Hadi Mwisho kwenye WhatsApp

WhatsApp ilibuniwa kwa kuzingatia wazo rahisi: unachoshiriki na familia na marafiki zako hakifai kutoka nje. Miaka mitano iliyopita, tuliongeza ufumbaji wa mwisho hadi mwisho. Kufikia sasa kipengele hicho hulinda zaidi ya ujumbe bilioni 100 kila siku wakati wa mawasiliano kati ya zaidi ya watumiaji bilioni 2.

Ingawa ujumbe uliofumbwa mwisho hadi mwisho unaotuma au kupokea huhifadhiwa kwenye kifaa chako, watu wengi pia wanataka mbinu ya kuhifadhi nakala za soga zao ili kuzipata endapo watapoteza simu zao. Kuanzia leo, tunazindua safu ya ziada ya hiari ya usalama ili kulinda kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, nakala za soga unazohifadhi kwenye Hifadhi ya Google au iCloud. Hakuna huduma nyingine ya mawasiliano ya ngazi ya ulimwengu inatoa kiwango hiki cha usalama kwa ujumbe, maudhui, ujumbe wa sauti, simu za video na nakala za soga za watumiaji.

Sasa unaweza kulinda nakala zako za soga zilizofumbwa mwisho hadi mwisho ukitumia nenosiri utakalojitungia au ufunguo wa usimbaji wenye tarakimu 64 ambao ni wewe pekee unaujua. WhatsApp wala mtoa huduma wako wa kuhifadhi nakala hawataweza kusoma nakala zako wala kufikia ufunguo unaohitajika kuzifungua.

Huku tukiwa na zaidi ya watumiaji bilioni 2, ni furaha yetu kuwapa watu chaguo zaidi za kulinda faragha yao. Tutazindua kipengele hiki polepole kwa watumiaji walio na toleo jipya zaidi la WhatsApp. Maelezo zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kulinda nakala zako kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye iOS na Android yanaweza kupatikana hapa, pia maelezo zaidi kuhusu jinsi tulivyobuni kipengele hiki yapo hapa.

TweetShiriki

Hamisha Soga Zako

Sasa Unaweza Kuhamishia Soga kwenye iPhone — MPYA, 7.20.22

Sasa unaweza pia kuhamisha soga zako zote za WhatsApp kutoka Android hadi iPhone unapobadilisha simu.

Hamishia kwenye Simu ya Android

Ni wewe unayemiliki ujumbe wako kwenye WhatsApp. Ndiyo maana ujumbe wako binafsi kwenye WhatsApp hulindwa kupitia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho na ndiyo maana tuna chaguo za kufanya ujumbe utoweke kiotomatiki kwenye soga zako.

Mojawapo ya vipengele ambavyo vimependekezwa sana ni kuwawezesha watumiaji kuhamisha soga kutoka mfumo mmoja wa uendeshaji hadi mwingine wanapobadilisha simu. Tumefanya jitihada kwa ushirikiano na watengenezaji wa vifaa na mifumo ya uendeshaji ili kusanidi kipengele hiki kwa njia salama na thabiti.

Tunafuraha kuzindua kipengele hiki kinachokuwezesha kuhamisha soga zako za WhatsApp kutoka iOS hadi Android. Hili hufanyika bila ujumbe wako kutumwa kwa WhatsApp na pia inajumuisha ujumbe wa sauti, picha na video. Kipengele hiki kinapatikana kwa vifaa vinavyotumia Android 12 na matoleo mapya zaidi.

Unapoweka mipangilio kwenye kifaa kipya, utapewa chaguo la kuhamisha soga zako kwa njia salama kutoka kwenye kifaa ulichokuwa ukitumia hadi kwenye kifaa kipya. Unahitaji kebo ya USB-C ambayo upande mmoja unaunganisha vifaa vya Apple (Lightning). Maelezo zaidi yanapatikana kwenye here.

Huu ni mwanzo tu. Tunatazamia kutoa kipengele hiki kwa watumiaji zaidi ili kuwawezesha kuhamia kwenye mifumo wanayopenda na kuhamisha soga zao kwa njia salama.

Mara ya Mwisho Kusasishwa: Julai 20, 2022

Tarehe 2 Septemba, 2021

TweetShiriki

Picha na Video za Kutazama Mara Moja

Ingawa kupiga picha na kurekodi video kwa simu zetu kumekuwa sehemu kubwa ya maisha yetu, si kila kitu tunachoshiriki kinafaa kuwa kumbukumbu ya kudumu ya kidijitali. Katika simu nyingi, ukipiga picha itachukua nafasi na kukaa katika hifadhi ya kamera yako daima.

Hii ndiyo sababu leo tunazindua picha na video za Kutazama Mara Moja ambazo zitatoweka kwenye soga baada ya kufunguliwa, hivyo kuwapa watumiaji uwezo zaidi wa kudhibiti faragha yao.

Kwa mfano, unaweza kutuma picha ya Kutazama Mara Moja ya nguo mpya unazojipima dukani, kutoa maoni ya haraka kuhusu jambo fulani, au taarifa fulani nyeti kama vile nenosiri la Wi-Fi.

Sawa na ujumbe mwingine wa binafsi unaotuma kwenye WhatsApp, maudhui ya Kutazama Mara Moja hufumbwa mwisho hadi mwisho kwa hivyo WhatsApp haiwezi kuyaona. Pia yatawekewa alama bayana ya aikoni ya “mara moja”.

Baada ya maudhui kutazamwa, ujumbe utaonekana ukiwa na neno “imefunguliwa” ili kuepusha mkanganyiko kuhusu kilichokuwa kikifanyika kwenye soga wakati wa maudhui hayo kutoweka.

Tunazindua kipengele hiki kwa kila mtu kuanzia wiki hii na tunatazamia kupata maoni kuhusu njia hii mpya ya kutuma maudhui ya faragha na yanayotoweka.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu jinsi ya kukijaribu hapa.

Tarehe 3 Agosti, 2021

TweetShiriki

Usikose tena simu ya kikundi

Katika kipindi ambapo wengi wetu tuko mbalimbali, hakuna kitu kizuri zaidi ya kujumuika na ndugu na marafiki katika simu ya kikundi. Pia hakuna kitu kibaya kama kutambua kwamba umekosa fursa hiyo adimu.

Jinsi umaarufu wa simu za vikundi unavyoendelea kukua, tumekuwa tukiboresha hali ya utumiaji kwa watumiaji wetu, huku pia tukiendelea kutoa usalama na faragha kupitia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.

Leo, tunaongeza uwezo wa kujiunga na simu ya kikundi, hata baada ya simu hiyo kuanza. Uwezo wa kujiunga na simu ikiwa tayari imeanza unaondoa ulazima wa kujibu simu ya kikundi pindi inapoanza. Hali hii inaleta haraka na urahisi kama wa mazungumzo ya ana kwa ana katika simu za vikundi kwenye WhatsApp.

Wakati mwingine mazungumzo mazuri zaidi hufanyika usipoyatarajia. Sasa, ikiwa mtu katika kikundi chako amekosa kupokea simu ilipopigwa, bado anaweza kujiunga wakati wowote anapopenda. Pia unaweza kuondoka kwenye simu na kujiunga tena wakati wowote mradi simu bado inaendelea.

Pia tumebuni skrini ya maelezo ya simu ili uweze kuona ni nani tayari amejiunga na nani amealikwa lakini bado hajajiunga. Kadhalika, ukigusa ‘puuza’ unaweza kujiunga baadaye kutoka kwenye kichupo cha simu kwenye WhatsApp.

Kipengele cha simu unazoweza kujiunga nazo kinazinduliwa leo na tunataraji kwamba watu wataanza kufurahia hali hii mpya.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu jinsi ya kuijaribu hapa.

Tarehe 19 Julai, 2021

TweetShiriki

CDC Spanish Language Vaccine Finder on WhatsApp

We’re honored by the opportunity to support the U.S. government’s sprint to get more Americans vaccinated for COVID-19 before the July 4 holiday, or as soon as they are able to do so.

People of all backgrounds rely on WhatsApp, though we know WhatsApp plays a particularly strong role with Spanish speaking communities in the United States. This new Spanish-language vaccine finder the CDC developed makes it easy to find a location to get the shot, order a free ride to get there, and get information.

It’s amazing what can be done with just a simple text messaging service. Throughout the last year we’ve worked with over 150 governments and health organizations, like WHO and now the CDC, to help counter misinformation, provide updates, and get people vaccinated to end this pandemic. Please help us spread the word to someone you know by tapping https://wa.me/18336361122?text=hola.


Localizador de vacunas de los CDC en WhatsApp disponible en español

Es un honor para nosotros tener la oportunidad de apoyar al gobierno de Estados Unidos en su carrera por lograr que una mayor parte de la ciudadanía se vacune contra el COVID-19 antes de la celebración del 4 de julio, o tan pronto como les sea posible.

Si bien personas de todos los orígenes confían en WhatsApp, sabemos que esta aplicación juega un papel particularmente importante en la comunidad hispanohablante de Estados Unidos. Con el nuevo localizador de vacunas que desarrollaron los Centros para el Control y la Prevención de Enfermedades (CDC, por sus siglas en inglés) y que está disponible en español, será más fácil buscar un lugar donde vacunarse, solicitar un traslado gratuito al centro de vacunación y recibir información.

Es increíble lo que se puede lograr con un simple servicio de mensajería de texto. Durante el último año, trabajamos con más de 150 gobiernos y organizaciones de salud, como la Organización Mundial de la Salud (OMS) y ahora los CDC, para ayudar a contrarrestar la desinformación, ofrecer actualizaciones y lograr que las personas se vacunen para terminar con esta pandemia. Por favor, visita el siguiente enlace y ayúdanos a difundir el mensaje entre tus contactos: https://wa.me/18336361122?text=hola.

June 21, 2021

TweetShiriki
Ukurasa Unaofuata
Pakua
Nembo Kuu ya WhatsApp
Nembo Kuu ya WhatsAppPakua
Huduma ZetuVipengeleBloguHadithiKwa Biashara
Sisi ni naniKutuhusuKaziKituo cha ChapaFaragha
Tumia WhatsAppAndroidiPhoneMac/PCWhatsApp Mtandaoni
Unahitaji Msaada?Wasiliana NasiKituo cha MsaadaVirusi vya Korona
Pakua

WhatsApp LLC 2023 ©

Masharti ya Huduma