Tarehe 7 Desemba 2022
Leo tunafurahi kuleta avata kwenye WhatsApp, njia mpya na ya kibinafsi ya kujieleza.
Avata yako ni toleo lako la kidijitali ambalo linaweza kuundwa kutoka kwa mabilioni ya michanganyiko ya mitindo tofauti ya nywele, vipengele vya uso na mavazi. Kwenye WhatsApp sasa unaweza kutumia avata yako iliyobinafsishwa kama picha yako ya wasifu au kuchagua moja ya vibandiko 36 maalum vinavyoangazia hisia na vitendo vingi tofauti.
Kutuma avata ni njia ya haraka na ya kufurahisha ya kushiriki hisia na marafiki na familia. Inaweza pia kuwa njia nzuri ya kujiwakilisha bila kutumia picha yako halisi ili ihisike kuwa ya faragha zaidi.
Kwa watu wengi hii itakuwa mara ya kwanza kuunda avata na tutaendelea kutoa uboreshaji wa mitindo ikiwa ni pamoja na mwanga, utiaji kivuli, muundo wa mitindo ya nywele, na zaidi ambayo yatafanya avata kuwa bora zaidi baada ya muda.
Tunatumai utafurahiya kuunda na kushiriki avata zako, ambazo zitakuwa zikitolewa kwa watumiaji kila mahali kuanzia leo.