Tarehe 24 Januari 2019
Mnamo Januari mwaka jana tulizindua programu ya WhatsApp Business, na sasa kuna zaidi ya biashara milioni tano zinazoitumia kusaidia wateja, kukuza biashara zao na kuhudumia jumuiya zao kote ulimwenguni. Tunafurahi kwamba tumesaidia mamilioni ya biashara kukua. Kwa mfano, nchini India, chapa ya macho ya Glassic ya Bengaluru imetuambia kuwa asilimia 30 ya mauzo yake mapya yanazalishwa kupitia WhatsApp Business.
Ili kusaidia kusherehekea mwaka wa kwanza wa WhatsApp Business, tunatangaza kwamba baadhi ya vipengele vyetu maarufu sasa vinaweza kutumika kwenye WhatsApp ya wavuti na kompyuta. Vipengele hivi ni pamoja na:
Kutumia vipengele hivi kwenye kompyuta husaidia biashara kuokoa muda na kuwajibu wateja wao haraka. Tunayo furaha kuendelea kukuza WhatsApp Business na kuanzisha vipengele vipya vinavyorahisisha wateja kupata na kujihusisha na biashara ambazo ni muhimu kwao.