Tarehe 15 Mei 2023
Shauku yetu ni kutafuta njia mpya za kusaidia kuweka ujumbe wako kuwa wa faragha na salama. Leo, tunafurahi kukuletea kipengele kipya tunachokiita Kufuli ya Soga, ambacho hukuwezesha kulinda mazungumzo yako na wandani kwa kukuongezea safu moja zaidi ya usalama.
Kufunga soga huondoa mfululizo wote wa mazungumzokwenye kikasha pokezi na kuuweka ndani ya folda yake ambayo inaweza tu kufikiwa kwa nenosiri la kifaa chako au kibayometriki, kama vile alama ya kidole. Pia huficha kiotomatiki maudhui ya soga hiyo katika arifa, vilevile.
Tunafikiri kipengele hiki kitakuwa kizuri kwa watu ambao wana sababu ya kushiriki simu zao mara kwa mara na mwanafamilia au nyakati zile ambapo mtu mwingine ameshikilia simu yako wakati soga maalum zaidi zinapofika. Unaweza kufunga soga kwa kugusa jina la mtu-binafsi au kikundi na kuchagua chaguo la kufunga. Ili kufungua soga hizi, vuta kikasha chako polepole na uweke nenosiri la simu yako au biometriska.
Katika kipindi cha miezi michache ijayo tutaongeza chaguo zaidi za Kufuli ya Soga, ikijumuisha kufunga vifaa vinavyotumika na kuunda nenosiri maalum la mazungumzo yako ili uweze kutumia nenosiri la kipekee tofauti na unalotumia kwa simu yako.
Waambie marafiki zako kuhusu Kufuli ya Soga, ambayo inaanza sasa.