Tarehe 20 Septemba 2023
Leo katika tukio letu la kimataifa la Mazungumzo mjini Mumbai tunaanzisha vipengele vipya ambavyo vitasaidia kuharakisha jinsi ya kufanya mambo ya biashara katika soga ya WhatsApp.
Hali za Soga za Haraka na Flows
Tunazindua Flows ili biashara ziweze kukupa matumizi zaidi kama vile kuchagua kiti chako cha treni kwa haraka, kuagiza chakula au kuweka miadi - haya yote bila kuacha soga yako. Unapotumia Flows, biashara zitaweza kutoa menyu tele na fomu zinazoweza kugeuzwa kukufaa zinazofanikisha mahitaji tofauti. Tutafanya Flows kupatikana kwa biashara kote ulimwenguni kwa kutumia Jukwaa la WhatsApp Business katika wiki zijazo.
Chagua Huduma yako ya Malipo
Tunarahisisha kukamilisha ununuzi moja kwa moja kwenye soga. Kuanzia leo, watu nchini India wanaweza kuongeza bidhaa kwenye rukwama zao na kutuma malipo wakitumia njia wanayochagua kutoka kwa programu zote za UPI zinazotumika, kadi za malipo na za mkopo na zaidi. Tunafurahi kufanya kazi na washirika Razorpay na PayU ili kufanya malipo kwa kitu kuwa rahisi kama kutuma ujumbe.
Biashara Zilizothibitishwa na Meta kwenye WhatsApp
Tunawezesha biashara kupokea uthibitishaji kutoka kwa Meta, ili kukusaidia kujua kuwa unapiga soga na biashara inayofaa. Ili kuwa Meta Verified (kupata uthibitishaji wa Meta), biashara zinaonyesha uhalisi wao kwa Meta na kupokea beji iliyothibitishwa, usaidizi wa akaunti ulioimarishwa na ulinzi dhidi ya uigaji. Kwa biashara zinazotaka kujisajili, Meta Verified itakuja na vipengele vya ziada vinavyolipiwa ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuunda ukurasa maalum wa WhatsApp ambao unaweza kutambulika kwa urahisi kupitia utafutaji wa wavuti, na usaidizi wa vifaa vingi ili wafanyakazi wengi waweze kujibu wateja. Tutaanza kujaribu Meta Verified hivi karibuni na wafanyabiashara wadogo wanaotumia programu ya WhatsApp Business kabla ya kuitambulisha kwa biashara kwenye Jukwaa la WhatsApp Business siku zijazo.
Tunayo furaha kuendelea kuunda vipengele bora kwa biashara ili kuboresha huduma kwa wateja na matoleo mengine wanayotoa kwa watu, na tunatarajia kusikia jinsi masasisho haya mapya yanavyosaidia kuanzisha miunganisho, kujenga mahusiano na kufanya mengi zaidi.