Tarehe 22 Machi 2023
WhatsApp ilianza kama programu ya simu na msingi huo unabaki kuwa imara kama zamani. Lakini kwa kuwa mamia ya mamilioni ya watu wanatumia WhatsApp kwenye kompyuta na kompyuta kibao, tunalenga katika kuboresha matumizi ya ujumbe na kupiga simu kwenye vifaa vyote.
Leo, tunaleta programu mpya kabisa ya WhatsApp ya Windows, inayoweza kupakuliwa hapa.
Programu mpya ya kompyuta ya dawati ya Windows hupakia haraka na imeundwa kwa kiolesura kinachojulikana kwa watumiaji wa WhatsApp na Windows. Unaweza kuanzisha simu za video za kikundi za hadi watu 8 na simu za sauti za hadi watu 32. Tutaendelea kuongeza idadi hizi muda baada ya muda ili uweze kuwasiliana na marafiki, familia na wafanyakazi wenzako kila wakati.
WhatsApp ndio jukwaa kubwa zaidi la kukupa matumizi kamili ya usimbaji fiche kutoka mwisho hadi mwisho ambayo inaruhusu mawasiliano ya majukwaa mbalimbali kati ya simu za mkononi, kompyuta, vipakatalishi na zaidi. Hii ina maana kwamba ujumbe wako wa kibinafsi, media na simu husimbwa kwa njia fiche kutoka mwisho hadi mwisho kwenye vifaa vyako vyote.
Tangu kuanzisha uwezo mpya wa vifaa vingi, tumesikiliza maoni na kufanya maboresho ikiwa ni pamoja na kuunganisha kifaa kwa haraka na usawazishaji bora kwenye vifaa vyote, pamoja na vipengele vipya kama vile onyesho la kukagua viungo na vibandiko.
Tunapoendelea kuongeza idadi ya vifaa vinavyotumia WhatsApp, tumeanzisha utumiaji mpya wa WhatsApp beta kwa vipakatalishi vya Android . Pia tunazindua programu mpya, yenye kasi zaidi kwa kompyuta za dawati za Mac ambayo kwa sasa iko katika hatua za mapema za beta.
Tunatazamia kuleta WhatsApp kwa vifaa vingi zaidi katika siku zijazo.