Tarehe 16 Aprili, 2024
Kufungua WhatsApp na kutafuta mazungumzo yanayofaa kunapaswa kuwa haraka, bila tatizo na rahisi. Kadiri watu wanavyozidi kufanya mengi kwenye WhatsApp, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kuweza kupata ujumbe wako haraka. Ndiyo maana leo tunazindua Vichujio vya Gumzo mpya ili uweze kufanya hivyo bila kulazimika kupitia kisanduku pokezi chako kizima.
Ili kuanza, unaweza kuchagua kati ya vichujio vitatu ambavyo vitaonekana juu ya orodha yako ya gumzo: Zote, Ambazo Hazijasomwa, Vikundi, ambavyo vinaweza kuchaguliwa kwa kugusa tu:
Tunaamini kuwa vichujio vitarahisisha watu kujipanga na kutafuta mazungumzo yao muhimu zaidi na kusaidia kupitia ujumbe kwa ufanisi zaidi. Tutaendelea kuunda chaguo zaidi ili kukusaidia kuzingatia yale yaliyo muhimu zaidi. Hizi zinaanza kutolewa kwa watumiaji leo, na zitapatikana kwa kila mtu katika wiki zijazo.