Tarehe 21 Machi 2023
Mwaka jana, tulizindua Jumuiya, ili kuwasaidia watu kunufaika zaidi kutoka katika vikundi vyao kwenye WhatsApp. Tangu kuzinduliwa, tumetaka kuunda nyenzo zaidi za wasimamizi na watumiaji pia. Leo tunafurahi kuzindua mabadiliko mapya machache ambayo tumefanya ili kurahisisha zaidi udhibiti na utumiaji wa vikundi kwa wasimamizi na kila mtu.
Vidhibiti vipya kwa wasimamizi
Watu wengi wanapojiunga na jumuiya, tunataka kuwapa wasimamizi wa vikundi udhibiti zaidi wa faragha ya kikundi chao, kwa hivyo tumeunda nyenzo rahisi ambayo inawapa wasimamizi uwezo wa kuamua ni nani anayeweza kujiunga na kikundi. Msimamizi anapochagua kushiriki kiungo cha mwaliko wa kujiunga na kikundi chao, au kufanya kikundi chao kuwa wazi kwa kujiunga katika jumuiya, sasa wana udhibiti zaidi wa nani anayeweza kujiunga. Vikundi ni mahali ambapo watu huwa na baadhi ya mazungumzo yao ya karibu zaidi na ni muhimu kwamba wasimamizi waweze kuamua kwa urahisi ni nani anayeweza na asiyeweza kuingia.
Ona kwa urahisi vikundi mnavyoshiriki
Pamoja na ukuaji wa Jumuiya na vikundi vyake vikubwa, tunataka kurahisisha kujua ni vikundi gani mnavyoshiriki na mtu mwingine. Iwe unajaribu kukumbuka jina la kikundi ambacho unajua unashiriki na mtu fulani au unataka kuona vikundi ambavyo nyote mko ndani, sasa unaweza kutafuta kwa urahisi jina la mtu unayemjua ili kuona vikundi vyenu kwa pamoja.
Vipengele hivi vitaanza kutumika duniani kote katika wiki zijazo, tunapoendelea kuunda nyenzo mpya za kufanya vikundi kuwa na hali bora zaidi kwa wasimamizi na wanachama kwa pamoja.