Watu wanapenda kupiga soga kwenye WhatsApp na biashara wanazopendelea, lakini kubadilishana jumbe na picha nyingi ili kupata maelezo ya bidhaa kunachosha. Leo tuna rahisisha kujifunza kuhusu bidhaa na huduma biashara zinazotoa kwa kutambulisha orodha kwenye programu ya WhatsApp Business.
Orodha ni rafu ya duka rununu kwa ajili ya biashara kuonyesha na kushirikisha bidhaa zao ili watu wanaweza kuvinjari kwa urahisi na kugundua kitu ambacho wangependa kununua. Zamani biashara zililazimika kutuma picha za bidhaa moja kwa wakati mmoja na kurudia kutoa maelezo - sasa wateja wanaweza kuona orodha yao kamili kwenye WhatsApp. Hii inawafanya wamiliki wa biashara waonekane kitaalamu zaidi na inawafanya wateja kujiingiza kwenye soga bila kutembelea tovuti.
Kama Agradaya, biashara endelevu ya mimea na viungo iliyo Indonesia. Tulimpa mwanzilishi Andhika Mahardika ufikiaji wa kipengele cha orodha mapema na alituambia kwamba kinafanya wateja wajifunze kirahisi kuhusu bidhaa zao, kujua bei na kuona picha za wanazotoa - hii ni muhimu kwa kuwahudumia wateja wao kwa ubora.
Kwa kila kitu kwenye orodha, biashara inaweza kuongeza habari pamoja na bei, maelezo na nambari ya bidhaa. WhatsApp inahudumia orodha hizi ili kuokoa nafasi muhimu ya hifadhi kwenye simu za biashara na wateja wote.
Kuunda orodha kwenye programu ya WhatsApp Business inachukua tu hatua chache. Tazama video ili kuanza:
Kipengele hiki cha orodha kinapatikana leo kwa biashara zinazotumia programu ya WhatsApp Business kwenye Android na iPhone nchini Brazil, Ujerumani, India, Indonesia, Mexico, Uingereza na Marekani. Itatandazwa duniani kote hivi karibuni. Hatuwezi kungojea kusikia jinsi orodha zinasaidia biashara ndogo kuungana na wateja wao na kukua.
Novemba 7, 2019