Tarehe 5 Novemba, 2020
Kufikia leo, ujumbe wa WhatsApp hukaa daima kwenye simu zetu. Ingawa hali hiyo ni muhimu katika kudumisha kumbukumbu kutoka kwa familia na marafiki zetu, ujumbe mwingi tunaotuma haufai kudumu milele.
Lengo letu ni kufanya mazungumzo kwenye WhatsApp yahisi kama mazungumzo ya ana kwa ana kadri inavyowezekana, hii ina maana kwamba hayafai kubaki milele. Ndiyo maana tunafuraha kukuletea chaguo la ujumbe unaotoweka kwenye WhatsApp.
Hali ya ujumbe unaotoweka ikiwa imewashwa, ujumbe mpya unaotumwa kwenye soga utatoweka baada ya siku 7, hivyo kufanya mazungumzo yawe mepesi na ya faragha zaidi. Katika soga ya mtu na mwenzake, yeyote kati yao anaweza kuwasha au kuzima hali ya ujumbe unaotoweka. Katika vikundi, wasimamizi watakuwa na udhibiti.
Tunaanza kwa siku 7 kwa sababu tunafikiri kwamba itatoa utulivu wa akili ukijua kuwa mazungumzo hayatahifadhiwa milele, na pia yatadumu kwa muda wa kutosha hivi kwamba hutasahau soga ilihusu nini. Orodha ya bidhaa za kununua au anwani ya ilipo duka uliyopokea siku chache zilizopita itaendelea kuwa unapoihitaji, kisha itatoweka wakati huihitaji. Unaweza kusoma zaidi, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuwasha hali ya ujumbe unaotoweka hapa.
Tunataraji watu watafurahia hali ya ujumbe unaotoweka, hali hii itaanza kupatikana kwa watumiaji kila mahali mwezi huu.