Oktoba 31, 2019
Mapema mwaka huu, tulizindua Touch ID na Face ID kwa iPhone ili kutoa safu ya ziada ya usalama kwa watumiaji wa WhatsApp. Leo, tunatambulisha uthibitishaji kama huo,unaokuruhusu kufungua programu na alama ya kidole chako, kwa simu za Android zilizowezeshwa. Kuiwezesha, gusa Mipangilio > Akaunti > Faragha > Kufuli cha alama ya kidole. Kuwasha Fungua na alama ya kidole, na thibitisha alama ya kidole chako.