Tarehe 30 Novemba 2023
Mapema mwaka huu tulianzisha Kufuli la Soga kusaidia watu kulinda mazungumzo yao nyeti zaidi. Leo tunazindua nambari ya siri, njia ya ziada ya kulinda soga hizo na kuifanya iwe ngumu kujua ikiwa mtu anaweza kufikia simu yako au unashiriki simu na mtu mwingine.
Ukiwa na nambari ya siri sasa utaweza kuweka nenosiri la kipekee tofauti na unalotumia kufungua simu yako ili kuzipa soga zako zilizofungwa safu ya ziada ya faragha. Utakuwa na chaguo la kuficha folda ya Soga Zilizofungwa kutoka kwa orodha yako ya soga ili ziweze kugunduliwa tu kwa kuandika nambari yako ya siri kwenye upau wa utafutaji. Ikiwa hiyo haitoshelezi mahitaji yako, bado unaweza kuchagua kuwa nazo kwenye orodha yako ya soga. Wakati wowote kuna gumzo jipya ambalo unataka kulifunga, sasa unaweza kubonyeza kwa muda mrefu ili kulifunga badala ya kutembelea mipangilio ya gumzo.
Tunafurahi sana kwamba jamii yetu imekuwa ikipenda Kufuli la Soga, na tunatumai kwamba nambari hiyo ya siri inafanya iwe muhimu zaidi kwao. Nambari ya siri inaanza kutolewa leo, na katika miezi ijayo itapatikana kote ulimwenguni. Tunafurahi kuendelea kuleta vipengele zaidi kwenye Kufuli la Soga ili kuwasaidia watu kulinda faragha yao, tupe maoni yako.