Tarehe 4 Februari 2019
Katika WhatsApp tunajali sana ujumbe wa kibinafsi, na leo tunafurahi kuzindua Touch ID na Face ID kwenye iPhone ili kumzuia mtu kuchukua simu yako na kusoma ujumbe wako.
Ili kuwezesha kipengele cha iPhone kwenye WhatsApp, gusa Mipangilio > Akaunti > Faragha > Kufuli ya Skrini na uwashe Touch ID au Face ID. Una chaguo la kuchagua muda kabla ya Touch ID au Face ID kuulizwa baada ya WhatsApp kufungwa.
Kipengele hiki kinapatikana kwenye iPhone 5s au toleo la baadaye na iOS 9 na zaidi kuanzia leo.