Tarehe 4 Mei 2023
Tunapoendelea kuboresha programu hii, leo tunakufahamisha kuhusu vipengele vipya vinavyokuja kwenye WhatsApp ambavyo tunatumai vitafanya soga zikufae na ziwe za kufana.
Masasisho mapya katika Kura
Tunaleta masasisho matatu mapya ya kura ili kusaidia vikundi kukusanya maelezo na kufanya maamuzi pamoja.
Kusambaza ikiwa na Manukuu
Kushiriki picha kwenye WhatsApp ni mojawapo ya njia rahisi zaidi za kuarifu marafiki na familia kuhusu maisha yako, na uwezo wa kusambaza maudhui inamaanisha kuwa unaweza kusambaza upya picha kwa haraka kutoka kwa kikundi kimoja cha miunganisho hadi kingine. Lakini wakati mwingine unaweza kukosa muda wa kuongeza muktadha kabla ya mtu kujibu.
Sasa unaposambaza maudhui ambayo yana manukuu, una chaguo la kuhifadhi, kufuta au kuandika upya ili kutoa maelezo ya ziada unaposhiriki picha kati ya soga. Unaweza pia kuongeza maelezo mafupi kwa picha na video unapozisambaza.
Kushiriki Hati ikiwa na Maelezo mafupi
Kama vile unaposhiriki picha au video, hati unazosambaza zinaweza kuhitaji maelezo kidogo. Iwe ni wakati wa kutuma makala ya gazeti au hati ya kazini, sasa una chaguo la kuongeza maelezo mafupi kabla ya kusambaza.
Masasisho haya yameanza kutolewa kwa watumiaji duniani kote na yatapatikana kwa kila mtu katika wiki zijazo.