Tarehe 22 Mei 2023
Iwapo utakuwa umefanya makosa, au kubadilisha tu mawazo yako, sasa unaweza kuhariri ujumbe wako uliotumwa.
Kuanzia kusahihisha tahajia rahisi hadi kuongeza muktadha wa ziada kwa ujumbe, tunafurahi kukuletea udhibiti zaidi wa soga zako. Unachohitaji kufanya ni kubonyeza kwa muda mrefu kwenye ujumbe uliotumwa na uchague 'Hariri' kutoka kwa menyu hadi dakika kumi na tano baadaye.
Jumbe zilizohaririwa zitaonyesha ‘zimehaririwa’ kando yake, ili wale unaowatumia ujumbe wafahamu masahihisho bila kuonyesha historia ya uhariri. Kama ilivyo kwa jumbe zote za kibinafsi, midia na simu, jumbe zako na uhariri unaofanya zinalindwa kwa usimbaji fiche kutoka mwanzo hadi mwisho.
Kipengele hiki kimeanza kutolewa kwa watumiaji duniani kote na kitapatikana kwa kila mtu katika wiki zijazo.