Tarehe 25 Aprili 2023
Mwaka jana, tulianzisha uwezo wa watumiaji duniani kote kutuma ujumbe kwa urahisi kwenye vifaa vyao vyote*, huku wakidumisha kiwango sawa cha faragha na usalama.
Leo, tunaboresha huduma yetu ya vifaa vingi zaidi kwa kuanzisha uwezo wa kutumia akaunti moja ya WhatsApp kwenye simu nyingi.
Kikiwa kipengele kinachoombwa sana na watumiaji, sasa unaweza kuunganisha simu yako kama mojawapo ya hadi vifaa vinne vya ziada, sawa na unapounganisha na WhatsApp kwenye vivinjari vya wavuti,tabuleti na kompyuta za mezani. Kila simu iliyounganishwa inaunganishwa na WhatsApp kivyake, na hivyo kuhakikisha kuwa ujumbe wako wa kibinafsi, maudhui na simu zimesimbwa kwa njia fiche kutoka mwisho hadi mwisho, na ikiwa kifaa chako cha msingi hakitumiki kwa muda mrefu, tunakuondoa kiotomatiki kutoka kwa vifaa vingine vyote.
Kuunganisha simu kama vifaa vinavyotumika hurahisisha kutuma ujumbe. Sasa unaweza kubadilisha kati ya simu bila kuondoka na kuendeleza gumzo kutokea mahali ulipoishia. Au ikiwa wewe ni mfanyabiashara mdogo, wafanyakazi wa ziada sasa wanaweza kujibu wateja moja kwa moja kutoka kwa simu zao chini ya akaunti ile ile ya WhatsApp Business.
Sasisho hili limeanza kutolewa kwa watumiaji duniani kote na litapatikana kwa kila mtu katika wiki zijazo.
Pia, katika wiki zijazo, tunaleta njia mbadala na inayoweza kufikiwa zaidi ya kuunganisha kwenye vifaa shirikishi. Sasa unaweza kuweka nambari yako ya simu kwenye Wavuti ya WhatsApp ili kupokea msimbo wa mara moja, ambao unaweza kutumia kwenye simu yako kuwezesha kuunganisha kifaa, badala ya kulazimika kuchanganua msimbo wa QR. Tunatazamia kuanzisha kipengele hiki kwa vifaa vingine zaidi katika siku zijazo.