Pakua
Vipengele
Kupiga simuUjumbeVikundiVituoMeta AIHaliUsalama
FaraghaBloguProgramuKituo cha UsaidiziKwa Biashara
Ingia
Pakua
Rudi kwenye Blogu
Blogu ya WhatsApp

Emoji za kuonyesha hisia, Kushiriki Faili za GB 2, Vikundi vya 512

Emoji za kuonyesha hisia kwenye WhatsApp zimeboreshwa zaidi kupitia kibodi nzima ya emoji inayojumuisha chaguo la rangi ya ngozi. Tuna furaha kuwaletea watumiaji chaguo zaidi wanazoweza kutumia kujieleza wanapopiga soga na familia na marafiki.

Kama tulivyotangaza mwezi uliopita maono yetu kuhusu Jumuiya kwenye WhatsApp, sasa mashirika, biashara, na vikundi vya watu wanaotangamana kwa ukaribu wanaweza kuwasiliana kwa njia salama na kutekeleza mambo wanayolenga kwenye WhatsApp. Maoni ambayo tumepokea kufikia sasa yamekuwa mazuri sana na tunatazamia kutoa vipengele vingi vipya kwa watumiaji.

Tunafuraha kutangaza kuwa emoji za kuonyesha hisia sasa zinapatikana kwenye toleo jipya zaidi la programu. Emoji hizi zinafurahisha, ni rahisi kutumia na zinapunguza soga katika vikundi. Tutaendelea kuziboresha kwa kuongeza emoji zaidi katika siku zijazo.

Pia, sasa unaweza kutuma faili za hadi GB 2 zilizolindwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye WhatsApp. Ukubwa huu umeongezwa kutoka kikomo cha awali cha MB 100 na tunaamini kuwa hili litawezesha ushirikiano kati ya biashara ndogo ndogo na vikundi vya shule. Tunapendekeza utumie WiFi kwa faili kubwa na utaona kipima muda unapopakia au kupakua ili ujue muda ambao uhamishaji wako utachukua.

Mojawapo ya maombi muhimu ambayo tumepokea mara nyingi ni chaguo la kuongeza watu zaidi kwenye soga. Kwa sasa tumeanza kwa kuwezesha hadi watu 512 kuongezwa kwenye kikundi. Kudumisha jumuiya binafsi, salama na za faragha kunahusisha majukumu mengi na tunaamini kuwa maboresha haya yatawezesha watu na vikundi kutangamana kwa ukaribu.

Tunatumai watu watafurahia masasisho haya na tunatarajia kutoa maboresho zaidi mwaka mzima.

Mara ya Mwisho Kusasishwa: tarehe 11 Julai, 2022

Mei 5, 2022

Pakua
Nembo Kuu ya WhatsApp
Nembo Kuu ya WhatsApp
Pakua

Huduma Zetu

VipengeleBloguUsalamaKwa Biashara

Sisi ni nani

Kutuhusu sisiKaziKituo cha ChapaFaragha

Tumia WhatsApp

AndroidiPhoneMac/PCWhatsApp Web

Unahitaji msaada?

Wasiliana NasiKituo cha MsaadaProgramuUshauri wa Usalama
Pakua

WhatsApp LLC 2026 ©

Sheria na Sera ya FaraghaSitemap