Tarehe 25 Februari 2019
Ni miaka 10 imepita tangu tuanzishe WhatsApp! Katika muongo mmoja uliopita, tumesikia kutoka kwa watu kote ulimwenguni wanaotumia WhatsApp kuwasiliana na wapendwa wao, kuungana na jumuiya zao na kujenga biashara. Hadithi hizi zinaendelea kututia moyo, na kusherehekea hatua hii muhimu, tunaangalia nyuma baadhi ya matukio yetu makuu zaidi ya miaka iliyopita.
Tunafurahia kuendelea kujenga vipengele vinavyofanya WhatsApp iwe rahisi zaidi na ya kutegemewa na kila mtu. Asante kwa watumiaji wetu wote kote duniani kwa kutembea nasi katika safari hii!