Tarehe 6 Aprili, 2021
WhatsApp inafahari kuzindua kifurushi kipya cha vibandiko kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) kinachoitwa “Vaccines for All.” Tunataraji kwamba vibandiko hivi vitawapa watu njia bunifu na ya kupendeza ya kuwasiliana na kueleza furaha, utulivu na matumaini wanayohisi kwa faragha kwa kuzingatia yanayowezekana kutokana na chanjo ya COVID-19 pamoja na kuonyesha shukrani zao kwa wahudumu wa afya ambao wameendelea na ushujaa wa kuokoa maisha katika kipindi hiki kirefu kigumu.
Tangu kuanza kwa janga hili, tumeshirikiana na zaidi ya mashirika 150 ya kitaifa, majimbo na serikali za mitaa, pamoja na mashirika kama vile WHO na UNICEF kutoa huduma za COVID-19 kwa njia ya simu ili kuwaunganisha zaidi ya watumiaji bilioni 2 na taarifa na nyenzo sahihi. Zaidi ya ujumbe bilioni 3 umetumwa kupitia nambari hizi za huduma kote duniani katika mwaka uliopita.
Kwa vile janga linaingia katika awamu mpya katika mataifa mengi, serikali zinatumia nambari hizi za huduma kwa simu ili kuwaunganisha raia na taarifa sahihi za chanjo na usajili kwa njia ya faragha katika mataifa kama vile Indonesia, Afrika Kusini, Argentina, Brazil na India. Nchini Indonesia, wafanyakazi 500,000 wa afya walijisajili kwa miadi yao ya chanjo kupitia huduma hii katika siku 5 za kwanza.
Tunataka kusaidia serikali na mashirika ya kimataifa kuwaunganisha watu wengi kote duniani na taarifa na huduma za chanjo kadri inavyowezekana, hasa katika maeneo yaliyo magumu kufikia au miongoni mwa makundi ya waliotengwa. Pia tumeondoa matozo yanayotokana na utumaji wa ujumbe kupitia API ya WhatsApp Business.
Tunapoendelea polepole kurejelea utangamano wa ana kwa ana katika baadhi ya nchi, tunataraji kwamba watu wataendelea kushiriki mawazo na hisia zao za faragha - pamoja na matumaini - na ndugu na marafiki zao wa karibu kwenye WhatsApp.
Kifurushi cha vibandiko vya “Vaccines for All” sasa kinapatikana kwenye WhatsApp.