WhatsApp ilibuniwa kwa kuzingatia wazo rahisi: unachoshiriki na familia na marafiki zako hakifai kutoka nje. Miaka mitano iliyopita, tuliongeza ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwa kawaida, ambao kufikia sasa kipengele hicho hulinda zaidi ya ujumbe bilioni 100 kila siku wakati wa mawasiliano kati ya zaidi ya watumiaji bilioni 2.
Ingawa ujumbe uliofumbwa mwisho hadi mwisho unaotuma au kupokea huhifadhiwa kwenye kifaa chako, watu wengi pia wanataka mbinu ya kuhifadhi nakala za soga zao ili kuzipata endapo watapoteza simu zao. Kuanzia leo, tunazindua safu ya ziada ya hiari ya usalama ili kulinda kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, nakala za soga unazohifadhi kwenye Hifadhi ya Google au iCloud. Hakuna huduma nyingine ya mawasiliano ya ngazi ya ulimwengu inatoa kiwango hiki cha usalama kwa ujumbe, maudhui, ujumbe wa sauti, simu za video na nakala za soga za watumiaji.
Sasa unaweza kulinda nakala zako za soga zilizofumbwa mwisho hadi mwisho ukitumia nenosiri utakalojitungia au ufunguo wa usimbaji wenye tarakimu 64 ambao ni wewe pekee unaujua. WhatsApp wala mtoa huduma wako wa kuhifadhi nakala hawataweza kusoma nakala zako wala kufikia ufunguo unaohitajika kuzifungua.
Huku tukiwa na zaidi ya watumiaji bilioni 2, ni furaha yetu kuwapa watu chaguo zaidi za kulinda faragha yao. Tutazindua kipengele hiki polepole kwa watumiaji walio na toleo jipya zaidi la WhatsApp. Maelezo zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kulinda nakala zako kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye iOS na Android yanaweza kupatikana hapa, pia maelezo zaidi kuhusu jinsi tulivyobuni kipengele hiki yapo hapa.