Vipengele
Kupiga simuUtumaji ujumbeVikundiVituoMeta AIHaliUsalamaVidhibiti vya mzazi
FaraghaBloguProgramuKituo cha UsaidizKwa Biashara
Ingia
Pakua
Pakua
Rudi kwenye Blogu
Blogu ya WhatsApp

Pata Ujumbe Haraka zaidi ukitumia Vichujio vya Gumzo

Kufungua WhatsApp na kutafuta mazungumzo yanayofaa kunapaswa kuwa haraka, bila tatizo na rahisi. Kadiri watu wanavyozidi kufanya mengi kwenye WhatsApp, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kuweza kupata ujumbe wako haraka. Ndiyo maana leo tunazindua Vichujio vya Gumzo mpya ili uweze kufanya hivyo bila kulazimika kupitia kisanduku pokezi chako kizima.

Ili kuanza, unaweza kuchagua kati ya vichujio vitatu ambavyo vitaonekana juu ya orodha yako ya gumzo: Zote, Ambazo Hazijasomwa, Vikundi, ambavyo vinaweza kuchaguliwa kwa kugusa tu:

  • Zote: Mwonekano chaguomsingi wa jumbe zako zote.
  • Hazijasomwa: Ni bora kwa wakati unaotaka kuona ni mazungumzo gani unahitaji kupata au kujibu. Inaonyesha ujumbe ambao umetiwa alama na wewe kuwa haujasomwa au bado haujafunguliwa, kwa hivyo unaweza kuyapa kipaumbele majibu yako.
  • Vikundi: Kipengele kilichoombwa sana, sasa soga zako zote za kikundi zitapangwa katika sehemu moja, ili kurahisisha kupata wale uwapendao iwe ni gumzo ya chajio na familia au kupanga likizo yako ijayo. Hii pia itaonyesha vikundi vidogo vya Jumuiya.

Tunaamini kuwa vichujio vitarahisisha watu kujipanga na kutafuta mazungumzo yao muhimu zaidi na kusaidia kupitia ujumbe kwa ufanisi zaidi. Tutaendelea kuunda chaguo zaidi ili kukusaidia kuzingatia yale yaliyo muhimu zaidi. Hizi zinaanza kutolewa kwa watumiaji leo, na zitapatikana kwa kila mtu katika wiki zijazo.

Tarehe 16 Aprili, 2024

Pakua
Nembo Kuu ya WhatsApp
Nembo Kuu ya WhatsApp
Pakua

Huduma zetu

  • Vipengele
  • Blogu
  • Usalama
  • Kwa ajili ya Biashara

Sisi ni nani

  • Kuhusu sisi
  • Taaluma
  • Kituo cha Chapa
  • Faragha

Tumia WhatsApp

  • Simu
  • Desktop
  • Kompyuta kibao
  • WhatsApp Web

Unahitaji msaada?

  • Wasiliana Nasi
  • Kituo cha Usaidizi
  • Programu
  • Ushauri wa Usalama
Pakua

WhatsApp LLC 2026 ©

Sheria na Sera ya FaraghaSitemap
  • Afrikaans
  • azərbaycan
  • Bahasa Indonesia
  • català
  • čeština
  • dansk
  • Deutsch
  • eesti
  • English
  • español
  • Filipino
  • français
  • Gaeilge
  • hrvatski
  • italiano
  • Kiswahili
  • latviešu
  • lietuvių
  • magyar
  • Melayu
  • Nederlands
  • norsk bokmål
  • o‘zbek
  • polski
  • Português (Brasil)
  • Português (Portugal)
  • română
  • shqip
  • slovenčina
  • slovenščina
  • suomi
  • svenska
  • Tiếng Việt
  • Türkçe
  • Ελληνικά
  • български
  • қазақ тілі
  • македонски
  • русский
  • српски
  • українська
  • עברית
  • اردو
  • العربية
  • فارسی
  • मराठी
  • हिन्दी
  • বাংলা
  • ਪੰਜਾਬੀ
  • ગુજરાતી
  • தமிழ்
  • తెలుగు
  • ಕನ್ನಡ
  • മലയാളം
  • ไทย
  • 한국어
  • 日本語
  • 简体中文
  • 繁體中文(台灣)
  • 繁體中文(香港)