Vipengele
Kupiga simuUtumaji ujumbeVikundiVituoMeta AIHaliUsalamaVidhibiti vya mzazi
FaraghaBloguProgramuKituo cha UsaidizKwa Biashara
Ingia
Pakua
Pakua
Rudi kwenye Blogu
Blogu ya WhatsApp

Masasisho mapya ya Kura na kusambaza pamoja na maelezo mafupi kwenye WhatsApp

Tunapoendelea kuboresha programu hii, leo tunakufahamisha kuhusu vipengele vipya vinavyokuja kwenye WhatsApp ambavyo tunatumai vitafanya soga zikufae na ziwe za kufana.

Masasisho mapya katika Kura

Tunaleta masasisho matatu mapya ya kura ili kusaidia vikundi kukusanya maelezo na kufanya maamuzi pamoja.

  • Unda kura za kupiga mara moja: Unapohitaji jibu la uhakika, tumeleta chaguo kwa watayarishi wa kura hiyo kuruhusu watu kupiga kura mara moja pekee. Zima tu 'ruhusu majibu mengi' wakati wa kutayarisha kura ya maoni.
  • Tafuta kura katika soga zako: Haiwezekani kila mara kujibu kura hapo hapo, na inaweza kuwa vigumu kupata kura ndani ya soga baadaye. Sasa, unaweza kuchuja ujumbe kwa kura, kama vile kwa picha, video au viungo. Kwenye skrini ya 'Soga', bonyeza 'Tafuta' na kisha 'Kura' ili kupata orodha ya matokeo yote.
  • Endelea kupata taarifa kuhusu matokeo ya kura ya maoni: Sasa utapokea arifa watu watakapopiga kura kwenye kura zako, ili uwe na masasisho ya majibu kwa urahisi.

Kusambaza ikiwa na Manukuu

Kushiriki picha kwenye WhatsApp ni mojawapo ya njia rahisi zaidi za kuarifu marafiki na familia kuhusu maisha yako, na uwezo wa kusambaza maudhui inamaanisha kuwa unaweza kusambaza upya picha kwa haraka kutoka kwa kikundi kimoja cha miunganisho hadi kingine. Lakini wakati mwingine unaweza kukosa muda wa kuongeza muktadha kabla ya mtu kujibu.

Sasa unaposambaza maudhui ambayo yana manukuu, una chaguo la kuhifadhi, kufuta au kuandika upya ili kutoa maelezo ya ziada unaposhiriki picha kati ya soga. Unaweza pia kuongeza maelezo mafupi kwa picha na video unapozisambaza.

Kushiriki Hati ikiwa na Maelezo mafupi

Kama vile unaposhiriki picha au video, hati unazosambaza zinaweza kuhitaji maelezo kidogo. Iwe ni wakati wa kutuma makala ya gazeti au hati ya kazini, sasa una chaguo la kuongeza maelezo mafupi kabla ya kusambaza.

Masasisho haya yameanza kutolewa kwa watumiaji duniani kote na yatapatikana kwa kila mtu katika wiki zijazo.

Tarehe 4 Mei 2023

Pakua
Nembo Kuu ya WhatsApp
Nembo Kuu ya WhatsApp
Pakua

Huduma zetu

  • Vipengele
  • Blogu
  • Usalama
  • Kwa ajili ya Biashara

Sisi ni nani

  • Kuhusu sisi
  • Taaluma
  • Kituo cha Chapa
  • Faragha

Tumia WhatsApp

  • Simu
  • Desktop
  • Kompyuta kibao
  • WhatsApp Web

Unahitaji msaada?

  • Wasiliana Nasi
  • Kituo cha Usaidizi
  • Programu
  • Ushauri wa Usalama
Pakua

WhatsApp LLC 2026 ©

Sheria na Sera ya FaraghaSitemap
  • Afrikaans
  • azərbaycan
  • Bahasa Indonesia
  • català
  • čeština
  • dansk
  • Deutsch
  • eesti
  • English
  • español
  • Filipino
  • français
  • Gaeilge
  • hrvatski
  • italiano
  • Kiswahili
  • latviešu
  • lietuvių
  • magyar
  • Melayu
  • Nederlands
  • norsk bokmål
  • o‘zbek
  • polski
  • Português (Brasil)
  • Português (Portugal)
  • română
  • shqip
  • slovenčina
  • slovenščina
  • suomi
  • svenska
  • Tiếng Việt
  • Türkçe
  • Ελληνικά
  • български
  • қазақ тілі
  • македонски
  • русский
  • српски
  • українська
  • עברית
  • اردو
  • العربية
  • فارسی
  • मराठी
  • हिन्दी
  • বাংলা
  • ਪੰਜਾਬੀ
  • ગુજરાતી
  • தமிழ்
  • తెలుగు
  • ಕನ್ನಡ
  • മലയാളം
  • ไทย
  • 한국어
  • 日本語
  • 简体中文
  • 繁體中文(台灣)
  • 繁體中文(香港)