Ni miaka 10 tangu tuanze WhatsApp! Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, tumesikia kutoka kwa watu duniani kote ambao wanatumia WhatsApp kuendelea kuwasiliana na wapendwa wao, kuungana na jamii zao, na kujenga biashara. Hadithi hizi zinaendelea kututia moyo, na kusherehekea jambo hili muhimu, tunaangalia matukio makubwa yaliyotokea katika miaka iliyopita.
Tunafurahia kuendelea kujenga vipengele vinavyofanya WhatsApp iwe rahisi na ya kutegemewa na kila mtu. Asante kwa watumiaji wetu wote kote duniani kwa kuungana nasi katika safari hii!