Tarehe 31 Oktoba 2024

Mapema mwaka huu tulianzisha vichujio vya gumzo kama njia ya kupata ujumbe kwa haraka zaidi. Watu wamefurahia sana kwamba vinakusaidia kufuatilia magumzo yako, na tunafurahi kuvibadilisha haraka kuwa Orodha.
Ukiwa na Orodha, sasa unaweza kuchuja magumzo yako kwenye kategoria maalum za chaguo lako. Iwe hiyo ni orodha ya familia, kazi au mtaa wako wa karibu, Orodha hukusaidia kuzingatia mazungumzo ambayo ni muhimu zaidi, unapoyahitaji.
Unaweza kuunda na kuhariri orodha zako kwa urahisi kwa kugusa + katika upau wa kichujio kilicho juu ya kichupo chako cha Magumzo, au hariri kwa kubonyeza orodha kwa muda mrefu.
Sawa na 'vipendwa' vyako, unaweza kuongeza vikundi na magumzo ya ana kwa ana kwenye orodha, na orodha yoyote utakayounda itaonekana kwenye upau wa kichujio.
Tunaanzisha Orodha kwa watumiaji leo, na zitapatikana kwa kila mtu katika wiki zijazo. Tunatazamia kupanua utendaji wa Orodha ili kukusaidia kuzingatia watu na mazungumzo ambayo ni muhimu zaidi.