Aprili 28, 2020
Janga la COVID-19 limemaanisha kwamba wengi wetu sasa tumetenganishwa na marafiki na familia. Matokeo yake, tunaona kwamba watu kote ulimwenguni wanageukia upigaji simu na video kwenye WhatsApp zaidi kuliko hapo awali. Simu za kikundi zimekuwa muhimu sana na watumiaji wetu wameuliza kuungana na watu wengi kwa mara moja. Kuanzia leo, tunaongeza mara mbili zaidi ya idadi ya washiriki unaoweza kuwa nao kwenye video au simu ya WhatsApp kutoka watu 4 hadi 8 kwa wakati mmoja.
Kwa mwezi uliopita, kwa wastani watu wametumia zaidi ya dakika bilioni 15 wakiongea kila siku kwenye simu za WhatsApp, ikiwa ni zaidi ya siku ya kawaida kabla ya janga. Na kama ilivyo kwenye ujumbe wa maandishi, simu hizo zote zimelindwa kwa ufumbaji wa mwisho-kwa-mwisho. Tumeunda upigaji simu wa kikundi kwa njia ambayo inafanya ipatikane kwa watumiaji wengi iwezekanavyo, ikiwa ni pamoja na watu wenye vifaa vya viwango vya chini na muunganisho wa kasi ya chini wa mtandao.
Tunajua watu wanaweza kuhitaji njia mbalimbali za kujiunga wakati wakiwa nyumbani, hiyo ndiyo sababu WhatsApp pia inapatikana kwenye Portal — ambayo watumiaji wengi wametuambia imekuwa njia nzuri ya kushiriki sebule zao na familia wakati huu wa karantini.
Kupata WhatsApp mpya, yenye kipimo cha juu cha washiriki kwenye simu za WhatsApp, washiriki wote kwenye simu wanahitajika kusasisha toleo la hivi karibuni la WhatsApp linalopatikana kwenye iPhone au Android leo. Waulize marafiki zako na familia kusasisha WhatsApp na kuijaribu.