Tarehe 21 Aprili 2020
Mabilioni ya vibandiko vinatumwa kila siku kwenye WhatsApp ili kuwasaidia watu kushiriki mawazo ya faragha na hisia bila ya kuandika hata neno moja. Tangu tulipozindua vibandiko miezi 18 iliyopita, vimekuwa mojawapo ya njia zinazokua kwa kasi za watu kuwasiliana kwenye WhatsApp.
Tunafurahia kufanya kazi na Shirika la Afya Duniani kuanzisha kifurushi cha kibandiko cha "Pamoja Nyumbani" ambacho kitawasaidia watu kuunganishwa wakati wote wa janga kubwa la COVID-19 na hata baadaye. Vibandiko kama hivi vinaweza kuwa vya kufurahisha, kuelemisha na vya kijumla, kuvunja vizuizi vya lugha, umri, na vingine.
Tunatumaini watu watafurahia kutumia vibandiko hivi kuwajulia hali wapendwa wao, haswa wale wanaojisikia wametengwa, wapweke na kuogopa. Kifurushi hiki kinatoa namna ya ubunifu ya kuwakumbusha watu kunawa mikono yao, kudumisha umbali, mazoezi na muhimu pia kusherehekea mashujaa wa matibabu na vilevile mashujaa wa kibinafsi katika maisha yetu.
Kifurushi cha kibandiko cha "Pamoja Nyumbani" sasa kinapatikana kwenye WhatsApp, ikiwa ni pamoja na maandishi kwenye lugha 9 - Kiarabu, Kifaransa, Kijerumani, Kiindonesia, Kiitaliano, Kireno, Kirusi, Kihispania na Kituruki.