Tarehe 6 Aprili 2021
WhatsApp inafahari kuzindua kifurushi kipya cha vibandiko kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) kinachoitwa “Vaccines for All.” Tunatarajia kwamba vibandiko hivi vitawapa watu njia bunifu na ya kupendeza ya kuwasiliana na kueleza furaha, utulivu na matumaini wanayohisi kwa faragha kwa kuzingatia yanayowezekana kutokana na chanjo ya COVID-19 pamoja na kuonyesha shukrani zao kwa wahudumu wa afya ambao wameendelea na ushujaa wa kuokoa maisha katika kipindi hiki kirefu na kigumu.
Tangu kuanza kwa janga hili, tumeshirikiana na zaidi ya mashirika 150 ya kitaifa, majimbo na serikali za mitaa, pamoja na mashirika kama vile WHO na UNICEF kutoa huduma za COVID-19 kwa njia ya simu ili kuwaunganisha zaidi ya watumiaji bilioni 2 na taarifa na nyenzo sahihi. Zaidi ya jumbe bilioni 3 zimetumwa katika njia hizi za usaidizi za kimataifa katika mwaka uliopita.
Kwa vile janga linaingia katika awamu mpya katika mataifa mengi, serikali zinatumia nambari hizi za huduma kwa simu ili kuwaunganisha raia na taarifa sahihi za chanjo na usajili kwa njia ya faragha katika mataifa kama vile Indonesia, Afrika Kusini, Argentina, Brazil na India. Nchini Indonesia, wafanyakazi wa matibabu 500,000 walijiandikisha kwa miadi yao ya chanjo kwenye huduma hii katika siku zake 5 za kwanza.
Tunataka kusaidia serikali na mashirika ya kimataifa kuwaunganisha watu wengi kote duniani na taarifa na huduma za chanjo kadri inavyowezekana, hasa katika maeneo yaliyo magumu kufikia au miongoni mwa makundi ya waliotengwa. Pia tumeondoa ada zinazotokana na kutuma ujumbe kupitia API yetu ya Biashara ya WhatsApp.
Tunaposonga polepole, katika baadhi ya nchi, kuelekea kuwa pamoja ana kwa ana, tunatumai watu wataendelea kushiriki mawazo na hali zao za faragha - na matumaini - na familia zao na marafiki wa karibu kwenye WhatsApp.
Kifurushi cha vibandiko vya “Vaccines for All” sasa kinapatikana kwenye WhatsApp.