Tarehe 30 Machi 2022
Tulipozindua huduma ya ujumbe wa sauti kwa mara ya kwanza mwaka wa 2013, tulijua kuwa itabadilisha jinsi watu wanavyowasiliana. Kwa kutumia muundo rahisi, tumefanya kurekodi na kutuma ujumbe wa sauti kuwa haraka na rahisi kama kuandika ujumbe. Kwa wastani, watumiaji wetu hutuma jumbe za sauti bilioni 7 kila siku kwenye WhatsApp, na jumbe hizi zote zinalindwa kupitia usimbaji fiche wa mwisho hadi mwisho ili kudumisha faragha na usalama wake kila wakati.
Tunafuraha leo kutangaza vipengele vipya vinavyoboresha utumaji wa ujumbe wa sauti kwenye WhatsApp. Haya ni pamoja na:
Ujumbe wa sauti umewawezesha watu kujieleza vyema zaidi kwa urahisi na haraka. Kuonyesha hisia au msisimko ukitumia maneno ni rahisi zaidi kuliko maandishi, na katika hali nyingi, ujumbe wa sauti ndiyo njia inayopendelewa ya mawasiliano kwenye WhatsApp. Ni rahisi kwa mtu yeyote kutumia - kwa wanafamilia wasiopendelea kuandika ujumbe, kwa marafiki wanaopenda kusimulia hadithi, kwa wenzako wanaohitaji kutiwa moyo, au unapotaka kusikia sauti ya mpendwa wako mwishoni mwa siku ndefu yenye uchovu.
Tunasubiri kwa hamu kuona wateja wetu wakijaribu vipengele hivi vipya vitakapotolewa katika wiki zijazo.