Vipengele
Kupiga simuUtumaji ujumbeVikundiVituoMeta AIHaliUsalamaVidhibiti vya mzazi
FaraghaBloguProgramuKituo cha UsaidizKwa Biashara
Ingia
Pakua
Pakua
Rudi kwenye Blogu
Blogu ya WhatsApp

Meta AI kwenye WhatsApp - Sasa Inatumia Lugha nyingi, Ubunifu Zaidi na ni Nzuri

Meta AI kwenye WhatsApp. Vipengele Vipya; Lugha na nchi zaidi.

Wakati Meta AI inaendelea kuboreka kwa kutumia vipengele na lugha mpya muhimu, tunafurahi kuleta kisaidizi hiki muhimu na cha ubunifu katika nchi zaidi kuanzia leo.

Upanuzi wa Kimataifa Unaoendelea

Meta AI inaweza kukusaidia kwa majibu, mawazo na msukumo. Sasa inapatikana katika nchi 22, ikiwa na nyongeza mpya zaidi zikitolewa sasa kwa kujumuisha Ajentina, Chile, Kolombia, Ekwado, Meksiko, Peru na Kameruni katika lugha kadhaa mpya zikiwemo Kifaransa, Kijerumani, Kihindi, Kiitaliano, Kireno na Kihispania na nyingine zaidi zinazokuja.

Wazia Hariri

Pia tunarahisisha kuunda picha yako bora na Meta AI kwa kufanya iwezekane kubadilisha na kuhariri picha kwa urahisi, kwa kujumuisha kuongeza au kuondoa vitu vilivyomo. Kwa kuanza, charaza "wazia" ili kuelezea picha yako na kisha ujibu kile Meta AI inatoa kwa kuiomba iongeze, ipunguze, au ihuishe picha hiyo jinsi unavyopenda. Wazia Hariri inapatikana kwa Kiingereza mwanzoni, na lugha zaidi zinakuja hivi karibuni.

Jiwazie Mwenyewe

Ikiwa umewahi kujiuliza jinsi unavyoweza kuonekana kama shujaa, au ulitaka kujaribu nywele au mavazi tofauti - sasa unaweza kujifikiria ukifanya chochote. Charaza tu "Niwazie mimi" kwenye gumzo na Meta AI ili kuanza. Baada ya kuweka mipangilio ya haraka, utaweza kuongeza kidokezo kama vile "Niwazie nikiwa nimevalia vazi la rangi ya waridi na kijani kibichi" na Meta AI itaunda picha yako katika tukio hilo lililobinafsishwa. Unaweza kuweka upya au kufuta picha zako za usanidi wakati wowote. Hii inapatikana katika toleo la beta nchini Marekani kwa sasa, ikiwa na lugha na nchi zaidi zikija hivi karibuni.

Tunafurahi kuendelea kushiriki uwezo na maendeleo mapya kutoka Meta AI na watu zaidi na zaidi kupitia WhatsApp. Kama ilivyo desturi yetu, simu na ujumbe wako wa binafsi husalia ukiwa umefumbwa mwisho hadi mwisho, kumaanisha kuwa hata WhatsApp au Meta haziwezi kuusoma wala kuusikiliza. Timu inajitahidi kuboresha majibu kwa Meta AI haraka na inaleta maboresho kila baada ya wiki mbili. Tungependa kusikia kutoka kwako, na kuona jinsi Meta AI imekusaidia kuwa mbunifu zaidi na kujieleza. Tutambulishe kwenye Threads na ushiriki ulichowazia.

Tarehe 23 Julai, 2024

Pakua
Nembo Kuu ya WhatsApp
Nembo Kuu ya WhatsApp
Pakua

Huduma zetu

  • Vipengele
  • Blogu
  • Usalama
  • Kwa ajili ya Biashara

Sisi ni nani

  • Kuhusu sisi
  • Taaluma
  • Kituo cha Chapa
  • Faragha

Tumia WhatsApp

  • Simu
  • Desktop
  • Kompyuta kibao
  • WhatsApp Web

Unahitaji msaada?

  • Wasiliana Nasi
  • Kituo cha Usaidizi
  • Programu
  • Ushauri wa Usalama
Pakua

WhatsApp LLC 2026 ©

Sheria na Sera ya FaraghaSitemap
  • Afrikaans
  • azərbaycan
  • Bahasa Indonesia
  • català
  • čeština
  • dansk
  • Deutsch
  • eesti
  • English
  • español
  • Filipino
  • français
  • Gaeilge
  • hrvatski
  • italiano
  • Kiswahili
  • latviešu
  • lietuvių
  • magyar
  • Melayu
  • Nederlands
  • norsk bokmål
  • o‘zbek
  • polski
  • Português (Brasil)
  • Português (Portugal)
  • română
  • shqip
  • slovenčina
  • slovenščina
  • suomi
  • svenska
  • Tiếng Việt
  • Türkçe
  • Ελληνικά
  • български
  • қазақ тілі
  • македонски
  • русский
  • српски
  • українська
  • עברית
  • اردو
  • العربية
  • فارسی
  • मराठी
  • हिन्दी
  • বাংলা
  • ਪੰਜਾਬੀ
  • ગુજરાતી
  • தமிழ்
  • తెలుగు
  • ಕನ್ನಡ
  • മലയാളം
  • ไทย
  • 한국어
  • 日本語
  • 简体中文
  • 繁體中文(台灣)
  • 繁體中文(香港)