Huwa tunajitahidi siku zote ili kufanya WhatsApp kuwa rahisi kutumia na kuwa ya kufurahisha zaidi, kwa hivyo tunafurahia kuanza mwaka mpya kwa vipengele mbalimbali vipya na maboresho ya muundo.
Camera effects: Ulipenda madoido tuliyoyazindua kwenye simu za video mwaka jana. Sasa, unapopiga na kutuma video au picha kwenye magumzo yako, unaweza kuchagua kutoka mandharinyuma, vichujio na madoido 30 sawa ili kubadilisha picha zako.
Selfie stickers: Kwa mashabiki wa vibandiko maalum, sasa unaweza kubadilisha selfi yako moja kwa moja kuwa kibandiko. Donoa tu kibandiko kwenye unda kibandiko na utaona chaguo la kamera la kupiga selfi na kuunda kibandiko chako. Inapatikana kwenye Android na inakuja kwa iOS hivi karibuni.
Share a sticker pack: Je, umeona kifurushi cha vibandiko unavyojua rafiki yako atapenda? Sasa unaweza kuvishiriki kwa urahisi moja kwa moja kwenye magumzo yako.
Quicker reactions: Sasa unaweza kudonoa ujumbe mara mbili ili kutoa hisia na kusogeza haraka hisia zako zinazotumiwa sana.
Tunatazamia kuleta vipengele zaidi vya kusisimua mwaka huu, huku tukitoa utumaji ujumbe wa faragha na salama popote ulipo duniani.