Tarehe 2 Septemba, 2021
Ni wewe unayemiliki ujumbe wako wa WhatsApp. Ndiyo maana ujumbe wako binafsi wa WhatsApp hulindwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho na ndiyo maana tunatoa njia za kufanya ujumbe utoweke kiotomatiki kutoka kwenye soga zako.
Mojawapo ya vipengele ambavyo tumeombwa sana ni kuwa na uwezo wa kuhamisha historia ya soga zako kutoka kwenye mfumo mmoja wa uendeshaji kwenda kwenye mwingine unapobadili simu. Tumefanya kazi kwa bidii kwa ushirikiano na watengenezaji wa mifumo ya uendeshaji na vifaa ili kubuni njia salama na ya uhakika.
Tunafurahi kuzindua uwezo wa kuhamisha historia yako ya WhatsApp kutoka kwenye iOS kwenda kwenye Android. Hili hufanyika bila ujumbe wako kutumwa kwenda kwa WhatsApp katika mchakato unaojumuisha ujumbe wa sauti, picha na video. Ili kuanza, kipengele hiki kinapatikana kwenye vifaa vya Samsung vinavyotumia Android 10 au matoleo ya baadaye na kitapatikana kwenye vifaa zaidi vya Android hivi karibuni.
Unapoweka mipangilio kwenye kifaa kipya, utapewa chaguo la kuhamisha soga zako kwa usalama kutoka kwenye kifaa chako cha zamani kwenda kwenye kifaa kipya. Mchakato huu unahitaji kebo ya USB-C ambayo upande mmoja unaunganisha vifaa vya Apple (Lightning). Unaweza kupata maelezo zaidi hapa.
Huu ni mwanzo tu. Tunatazamia kufanya chaguo hili lipatikane kwa watu wengi zaidi ili waweze kuhamia kwenye mifumo wanayopenda na kwenda na soga zao kwa usalama.