Vipengele
Kupiga simuUtumaji ujumbeVikundiVituoMeta AIHaliUsalamaVidhibiti vya mzazi
FaraghaBloguProgramuKituo cha UsaidizKwa Biashara
Ingia
Pakua
Pakua
Rudi kwenye Blogu
Blogu ya WhatsApp

Tafuta, Tuma ujumbe na Nunua kwenye WhatsApp

Leo tunashiriki toleo jipya kuhusu kile tunachounda ili kuwasaidia watu kupata, kutuma ujumbe na kununua kitu kutoka kwa biashara kwenye WhatsApp. Timu yetu iko nchini Brazil leo ambapo tunajadili maono yetu ya kuleta hali yote ya ununuzi moja kwa moja kwenye gumzo la WhatsApp.

Tafuta biashara

Watu wanataka njia rahisi ya kupata usaidizi kwa haraka kutoka kwa mamilioni ya biashara ndogo ndogo na makumi ya maelfu ya biashara ambazo tayari ziko kwenye WhatsApp. Leo tunazindua uwezo wa kupata biashara moja kwa moja kwenye WhatsApp ili watu sasa waweze kuvinjari biashara kulingana na aina - kama vile usafiri au benki - au utafutaji kwa jina la biashara. Hii itaokoa watu dhidi ya kutafuta nambari za simu nje ya tovuti au kuandika nambari kwenye waasiliani wao.

Tumeunda utafutaji wa biashara kwa njia ambayo inahifadhi usiri wa watu. Unachotafuta huchakatwa kwa njia ambayo hakiwezi kuunganishwa kwa akaunti yako. Mwanzo, tunaleta uwezo wa kutafuta biashara nchini Brazili, Kolombia, Indonesia, Meksiko na Uingereza ambako watu wanaweza kupata kampuni za kibiashara kwa kutumia Mfumo wetu wa Biashara wa WhatsApp. Nchini Brazili, utafutaji utasaidia watu kupata biashara ndogo ndogo pia.

Ujumbe

Biashara nyingi zinapotumia WhatsApp, suala la kipaumbele kwetu ni kuwaweka watu katika udhibiti wa mazungumzo yao. Kutenda ipasavyo ni muhimu kwa WhatsApp kama vile tu kwa watu na biashara zinazotutegemea. Baadhi ya biashara za hivi majuzi ambazo zimejiunga na WhatsApp zinawasaidia watu kufungua akaunti ya benki, kununua tikiti zao za usafir na kuagiza bidhaa.

Nunua

Hatimaye tunataka watu waweze kufanya malipo kwa usalama kutokea kwenye gumzo kwa kadi zao za mkopo au za malipo. Hivi majuzi tulizindua hali hii nchini India na tuna furaha kwa sasa kujaribu hili nchini Brazili na washirika wengi wa malipo. Utumiaji huu wa malipo usiofumwa utabadilisha jinsi watu na biashara zinazotaka kununua na kuuza kwenye WhatsApp bila kulazimika kwenda kwenye tovuti, kufungua programu nyingine au kulipa

Hali hizi mpya ni sehemu ya kufanya WhatsApp kuwa njia bora zaidi ya watu kuunganishwa na biashara zao wanazozipenda. Tunatazamia maoni yako.

Tarehe 17 Novemba, 2022

Pakua
Nembo Kuu ya WhatsApp
Nembo Kuu ya WhatsApp
Pakua

Huduma zetu

  • Vipengele
  • Blogu
  • Usalama
  • Kwa ajili ya Biashara

Sisi ni nani

  • Kuhusu sisi
  • Taaluma
  • Kituo cha Chapa
  • Faragha

Tumia WhatsApp

  • Simu
  • Desktop
  • Kompyuta kibao
  • WhatsApp Web

Unahitaji msaada?

  • Wasiliana Nasi
  • Kituo cha Usaidizi
  • Programu
  • Ushauri wa Usalama
Pakua

WhatsApp LLC 2026 ©

Sheria na Sera ya FaraghaSitemap
  • Afrikaans
  • azərbaycan
  • Bahasa Indonesia
  • català
  • čeština
  • dansk
  • Deutsch
  • eesti
  • English
  • español
  • Filipino
  • français
  • Gaeilge
  • hrvatski
  • italiano
  • Kiswahili
  • latviešu
  • lietuvių
  • magyar
  • Melayu
  • Nederlands
  • norsk bokmål
  • o‘zbek
  • polski
  • Português (Brasil)
  • Português (Portugal)
  • română
  • shqip
  • slovenčina
  • slovenščina
  • suomi
  • svenska
  • Tiếng Việt
  • Türkçe
  • Ελληνικά
  • български
  • қазақ тілі
  • македонски
  • русский
  • српски
  • українська
  • עברית
  • اردو
  • العربية
  • فارسی
  • मराठी
  • हिन्दी
  • বাংলা
  • ਪੰਜਾਬੀ
  • ગુજરાતી
  • தமிழ்
  • తెలుగు
  • ಕನ್ನಡ
  • മലയാളം
  • ไทย
  • 한국어
  • 日本語
  • 简体中文
  • 繁體中文(台灣)
  • 繁體中文(香港)